Padre John Maina: Picha Zaonesha Ziara ya Gachagua katika Parokia ya Igwamiti Kasisi Akiuawa

Padre John Maina: Picha Zaonesha Ziara ya Gachagua katika Parokia ya Igwamiti Kasisi Akiuawa

  • Rigathi Gachagua na Padre John Maina walionekana pamoja wakati wa hafla ya hivi majuzi kanisani
  • Wiki tatu tu baadaye, padri huyo alipatikana akiwa ametupwa baada ya kutekwa nyara na akafariki dunia alipokuwa akipokea matibabu
  • Habari hizo zimewaacha wengi wakiwa na mshangao, kwani hakuna aliyetarajia kifo cha padri kuhusishwa na siasa

Kifo cha Mchungaji John Maina kimeiacha nchi na hasa wananchi wa Igwamiti wakiwa wamesikitika pakubwa.

Padre John Maina: Picha Zaonesha Ziara ya Gachagua katika Parokia ya Igwamiti Padre Akiuawa
Padre John Maina alionekana nyuma ya Gachagua wakati wa ziara ya hivi majuzi Igwamiti. Picha: Rigathi Gachagua.
Chanzo: Facebook

Hii pia inaongeza kwenye orodha ndefu ya mauaji ambayo yamekuwa yakitokea nchini, huku Wakenya wakizidi kuhoji usalama wao katika taifa lao.

Padri John Maina alikufaje?

Kulingana na ripoti, padri huyo wa Kanisa Katoliki aliyehudumu Nyandarua aliuawa wiki tatu baada ya kuwa mwenyeji wa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua katika hafla moja.

Padri huyo kutoka Parokia ya Katoliki ya Igwamiti anaripotiwa kutekwa nyara na kushambuliwa kwa kifaa butu.

Mwili wake ulipatikana umetupwa kando ya barabara eneo la Kikopey, Gilgil, takriban kilomita 50 kutoka parokia aliyokuwa akihudumu.

Maina anaripotiwa kufariki dunia alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph, Gilgil.

Rigathi Gachagua na John Ndegwa walikutana lini?

Rigathi Gachagua alikuwa miongoni mwa wageni waliokuwa katika hafla ya maadhimisho ya miaka 25 ya Parokia ya St. Louis - Igwamiti.

TUKO.co.ke ilifanya upekuzi na kupata picha za hafla hiyo, baadhi zikimwonyesha Padri John Maina akiwa mwenye furaha alipowakaribisha viongozi katika parokia yake.

Gachagua alielezea jinsi ibada hiyo ilivyokuwa ya kupendeza, na aliongeza kuwa alizungukwa na joto la upendo wa kijamii na imani.

Hizi hapa ni picha kutoka kwa hafla hiyo: Wakenya waonyesha hisia zao kuhusu mauaji ya John Maina

Wakenya walishiriki hisia zao za mshangao na huzuni kutokana na mauaji hayo, huku wengine wakifariji familia na marafiki waliompoteza mpendwa wao.

itsmssuzzy kwenye IG alisema:

"Tumeifikia wapi kama taifa?"

patoo.006 kwenye IG alisema:

"Watu wanasahau kuwa nao pia watakufa na hukumu yao itafika."

lukengirubiu kwenye X alisema:

"Pole sana kwa dayosisi ya Katoliki ya Nyahururu na familia ya marehemu, mwanga wa milele umwangazie."

@oscar_konte kwenye X alisema:

"Tunatoa pole sana kwa familia na marafiki."

@CHARLESKAB38747 kwenye X alisema:

"Roho yake ipumzike kwa amani."

@njunge_josphat kwenye X alisema:

"Tunamwomboleza... apumzike kwa amani ya milele."

Kuria Thuo kwenye Facebook alisema:

"Wadi ya Gathanji inaomboleza kifo cha ghafla cha baba yetu wa kiroho Maina Ndegwa ambaye hadi kifo chake alikuwa akihudumu kwa waumini wa Kanisa Katoliki la St Louis Boiman, Wadi ya Gathanji. Nimepoteza rafiki mkubwa. Siku ya hukumu yaja. Kwaheri rafiki yangu Fr Maina."

Wakenya waomboleza kifo cha John Maina huku uchunguzi ukianzishwa

TUKO.co.ke iliripoti awali kuwa Wakenya walimwomboleza padri huyo kupitia mitandao ya kijamii huku uchunguzi kuhusu kifo chake ukiendelea.

Maafisa wa DCI wanashuku kuwa mwili wa padri huyo ulitupwa umbali mkubwa kutoka eneo alikouawa.

Uchunguzi wa maiti utafanyika katika Hospitali ya Misheni ya Katoliki ya Mtakatifu Benedict ili kutoa mwanga zaidi katika uchunguzi wa mauaji hayo.

Gari la padri huyo aina ya Subaru Forester pia linahusishwa na kutumika na wauaji wake kusafirisha mwili wake.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »