George Ruto Aonekana Barabarani Akipiga Picha Matatu ya MoneyFest Kisiri

George Ruto Aonekana Barabarani Akipiga Picha Matatu ya MoneyFest Kisiri

  • George Ruto alinaswa kwenye video ya mtandaoni akirekodi matatu yake ya MoneyFest ikitembea barabarani
  • Mtoto wa rais alikuwa amevalia kawaida katika jezi nyeupe ya Ziggo, jeans, sneakers na kofia
  • Kwa kuzingatia video hiyo, hakukuwa na walinzi wowote walioonekana kuwa naye labda tu kama walikuwa wakimchnga kwa mbali

Mwanawe Rais William Ruto George ameonekana mitaani.

George Ruto Aonekana Barabarani Akipiga Picha Matatu ya MoneyFest Kisiri
George Ruto alionekana katika mitaa ya Nairobi. Picha: George Ruto.
Chanzo: Instagram

George alipigwa picha akiinasa kwenye kamera matatu yake, MoneyFest, iliyokuwa ikipita barabarani.

Alikuwa amevalia jezi nyeupe yenye chapa ya Ziggo, jeans na sneakers pamoja na kofia.

Katika kanda hiyo, mwanawe rais alionekana akirekodi gari lililokuwa likisonga huku akijipanga kwa makini kupata pembe bora zaidi ya picha.

Hakuwa na walinzi karibu naye — huenda walikuwa wakimchunga kwa mbali. Vijana wachache walionekana walimzunguka alipokuwa akirekodi kwa simu yake.

Hii si mara ya kwanza George kuonekana hadharani akiwa peke yake. Miezi michache iliyopita, alipigwa picha akiendesha basi lake la MoneyFest kuelekea Rongai.

Kanda hiyo ilichapishwa na Matrix Family na ujumbe:

"Man like George kwa ground. Only The Family."

Kama ilivyotarajiwa, Wakenya wengi waliitikia klipu hiyo kwa mitazamo tofauti, lakini wengi walimsifu George kwa unyenyekevu wake.

Haya hapa ni baadhi ya maoni yaliyotolewa:

@stalk_c_ity: "Simple man huyu. At least hatutasahau hizi good days."

@vegxs: "Very Humble Man on ground."

@i_aint_your_boy: "Man like George. Achezee kaa yeye bana apo kwa ao wasee wa NTSA."

@lucky_thrift1: "Prezzo anafaa apatie Georgy hiyo platform ya NTSA tunaeza kua na changes kwa hizi rules za 90's zibadilishwe manze."

George Ruto anasomea nini?

Jumanne, Aprili 15, Rais William Ruto aliwakaribisha kikosi cha timu ya taifa ya vijana walio chini ya umri wa miaka 20, Rising Stars, katika Ikulu ya Nairobi kabla ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri.

Rais alisifu vipaji na juhudi za timu hiyo, akifichua kuwa mwanawe George ni shabiki mkubwa wa michezo.

Alitangaza pia kuwa George anaendelea na masomo ya juu ng’ambo.

Rais Ruto aliahidi kuisaidia timu hiyo na kusema atahudhuria fainali iwapo watafika hatua huko.

Ruto aliongea kwa furaha kuhusu jinsi George amekuwa akimhimiza kuwekeza zaidi kwenye maendeleo ya michezo humu nchini.

Kwa sasa, George anasomea shahada ya uzamili katika usimamizi wa michezo (Sports Management).

George Ruto aonyesha kuwa yeye ni kiongozi mnyenyekevu

Kama tulivyokueleza awali, George alionekana akiwa na makanga na madereva wa matatu.

Jumapili, Aprili 20, picha zilisambaa zikionyesha George, ambaye pia ni mwekezaji katika sekta ya uchukuzi, akiwa na wahudumu wa matatu zake mbili — Matrix na MoneyFest.

Picha hizo zilizochukuliwa katika mazingira yenye mandhari nzuri zilionyesha madereva na makanga wameketi kwenye miamba ya zege, huku George akiwa nyuma yao amevaa jezi nyeusi ya Arsenal na kuonyesha kidole cha gumba juu kwa ishara ya pongezi.

Matatu hizo mbili, Matrix na MoneyFest, ni magari ya usafiri wa umma maarufu yanayoendesha katika barabara ya Embakasi jijini Nairobi chini ya chapa ya Raptor Family.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »