Milly Wa Doc: Video Ya Kipekee Bintiye TikToker Sheila Akimuomboleza Mamake Yaibuka
- Mipango ya mazishi na kumuaga TikToker Milly Wa Doc inaendelea, huku leo ikiwa ni siku ya tano tangu kifo chake kitokee
- Familia na marafiki wa mtayarishaji huyo wa maudhui wamekuwa wakikutana nyumbani kwake kujadili maandalizi ya mazishi
- Watu wengi mitandaoni walifurahishwa kumuona bintiye Milly kwa mara ya kwanza na wakaombea faraja ya Mungu katika maisha yake
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Bintiye marehemu TikToker Milly Wa Doc ameonekana huku mipango ya mazishi ya mamake ikiendelea.

Chanzo: TikTok
Binti huyo mchanga amekuwa akiishi maisha ya faragha, jambo sawia na mume wa mamake pamoja na mtoto wake wa kwanza wa kiume.
Kwa umma, ilikuwa wazi kuwa Milly aliwapenda watoto wake sana na aliwatakia mazuri, mara nyingi akiwapongeza kwa jinsi walivyokomaa kimwili na kiakili pia.
Hata hivyo, Milly alijitahidi kuwaweka mbali na macho ya umma ili kuwalinda na kuhakikisha wanaishi maisha yao kwa uhuru.
Video moja ikionyesha binti ya Milly akiomboleza kifo cha mamake imeibuka kwenye mitandao ya kijamii siku chache baada ya kifo cha mtayarishaji huyo wa maudhui.
Katika video hiyo, Sheila, ambaye inasemekana ana baba Mjerumani, alionekana akiwa na huzuni kubwa akiwa na jamaa wengine wa familia.
Familia ilikuwa imekusanyika kuomboleza na pia kupanga mipango ya mazishi ya marehemu, aliyefariki Jumatatu, Juni 2 kutokana na matatizo ya kiafya.
Sheila alionekana kuwa mwenye huzuni tele na rafiki mmoja alionekana akimfariji ili kumpa nguvu katika wakati huo mgumu.
Wengi waliotazama video hiyo walituma rambirambi zao kwa familia hiyo, wakitumai watapata faraja kutoka kwa Mungu.
Haya hapa ni baadhi ya maoni yaliyokusanywa na TUKO.co.ke:
chepchumba alisema:
"Mungu, tafadhali walinde na umpe mama yao pumziko la amani."
Leah Nimo alisema:
"Mungu najua mimi si mkamilifu lakini nakuomba nipe muda wa kutosha kulea watoto na wajukuu wangu."
Bella bella alisema:
"Mungu, kwa ajili ya watoto wetu, tusife tukiwa bado wachanga."
hellennjoki297 alisema:
"Aki si baba Shayla akuje achukue hawa watoto akae nao. Mungu wangu wafariji."
rayban alisema:
"Nimeshindwa hata kusema. Nilikuwa mfuasi wa Milly lakini siwezi kueleza, nalia sana 😭 Milly, umewaachia nani hawa watoto katika dunia hii ya leo, mama?"
chloeshanno alisema:
"Mungu amlinde Sheila na Brian."
gamarblack sheep alisema:
"Ni hadi unapofariki ndio nyumba yako inajaa watu ambao hawakuwepo ulipokuwa na msongo wa mawazo na hawakukusaidia. Pumzika kwa amani."
being_ninah alisema:
"Mungu awalinde hawa watoto, aki."

Chanzo: TikTok
Ujumbe wa mwisho wa Milly kwa watoto wake
Kama ilivyoripotiwa awali, video ya Milly akiwapongeza watoto wake ilijitokeza tena baada ya kifo chake.
Akizungumza na TUKO.co.ke, Milly alieleza kwa fahari jinsi alivyojivunia watoto wake, Brian na Sheila.
Alisema anajua anamlea kijana wa heshima katika Brian na malkia katika Sheila, huku akiwashukuru kwa kusimama naye katika nyakati ngumu.
Pia alisimulia hadithi ya kusikitisha kuhusu jinsi mwanaye wa kiume alilia kwa furaha baada ya kupata nafasi ya kushiriki mlo naye mezani kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke