Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi

Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi

  • Huduma ya Kitaifa ya Polisi imetangaza kumsimamisha kazi na kuwatia mbaroni maafisa wawili wa polisi wanaohusishwa na kupigwa risasi kwa mchuuzi wakati wa maandamano
  • Konstebo Klinzy Barasa Masinde na Duncan Kiprono walikamatwa kufuatia tukio la kupigwa risasi kwa Boniface Mwangi Kariuki nje ya jengo la Imenti House
  • Ingawa wakili wa Barasa alikana kuwa afisa huyo alifyatua risasi ya mpira, Wakenya waliomtambua kwenye mitandao ya kijamii walimiminika kwenye kurasa zake wakitaka ajibu tuhuma hizo

Mnamo Jumatano, Juni 18, Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilitangaza kuwasimamisha kazi na kuwatia mbaroni konstebo wawili wa polisi.

Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi
Klinzy Barasa Masinde ni mmoja wa polisi wawili waliosimamishwa kazi baada ya kupigwa risasi Boniface Mwangi Kariuki. Picha: Klinzy Barasa.
Chanzo: Instagram

Klinzy Barasa Masinde na Duncan Kiprono walikamatwa wakati wa uchunguzi kuhusu kupigwa risasi kwa muuzaji wa barakoa Jumanne, Juni 17, wakati wa maandamano yaliyofanyika kulalamikia kifo cha Albert Ojwang akiwa mikononi mwa polisi.

TUKO.co.ke imekusanya picha za afisa huyo, ambaye hupenda kupakia machapisho kwenye mitandao ya kijamii.

1. Kwa nini Klinzy Barasa yuko matatani?

Video ya tukio hilo ilionyesha maafisa hao wawili wakimkabili Boniface Mwangi Kariuki karibu na Imenti House.

Kariuki alikuwa ameshika barakoa mkononi mwake mmoja na mkono mwingine ameuinua kujikinga.

Alionekana kujaribu kujiondoa lakini ghafla akaanguka chini, ambapo inadaiwa Barasa alifyatua risasi.

Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi
Klinzy Barasa alikamatwa. Picha: Klinzy Barasa.
Chanzo: Instagram

2. Wakenya walimtambuaje Klinzy Barasa?

Wakati wa tukio hilo, Barasa alikuwa amefunika uso wake kwa mavazi ya balaclava.

Hata hivyo, Wakenya walioko kwenye mtandao wa X walichunguza kwa haraka na picha za awali za Barasa kabla hajafunika uso zikaibuka.

Wadadisi wa mitandaoni walizidi hatua hiyo kwa kutambua majukwaa yake ya mitandao ya kijamii.

Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi
Wakenya walimtafuta mitandaoni hadi kumpata Klinzy Barasa. Picha: Klinzy Barasa.
Chanzo: Instagram

3. Wakenya walichukuliaje tukio hilo?

Tukio hilo lilikosolewa pakubwa na raia wa kawaida pamoja na watu maarufu.

Wengi walilalamikia ukosefu wa utu na huruma kutoka kwa maafisa wa polisi wa Kenya.

Kisa hiki kilielekeza tena macho ya umma kwa suala la ukatili wa polisi.

4. Wakili wa Klinzy Barasa alisema nini?

Kupitia wakili wake Felix Kiprono Keaton, Barasa alikana kuwa risasi ya mpira iliyompata Kariuki ilitoka kwenye bunduki yake.

Alidai kuwa ni tukio la kuchanganyikiwa kwa utambulisho.

Wakili huyo alitoa wito kwa Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) kuchukua jukumu la uchunguzi huo, akieleza mashaka kuhusu ushiriki wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI).

Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi
Klinzy Barasa alipinga madai ya kumpiga risasi muuza barakoa jijini Nairobi. Picha: Klinzy Barasa.
Chanzo: Instagram

5. Uwepo wa Klinzy Barasa kwenye mitandao ya kijamii

Barasa ana zaidi ya wafuasi 1,000 kwenye Instagram na mara kwa mara hupakia picha akiwa amevalia sare za polisi.

Chapisho lake la hivi karibuni lilimwonyesha akiwa na sare ya buluu ya polisi na jina lake likiwa limebandikwa.

Aliandika: "Siwezi kurekebisha ujinga, lakini naweza kuufunga."

Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi
Klinzy Barasa alikuwa hai sana kwenye mitandao ya kijamii. Photo: Klinzy Barasa.
Chanzo: Instagram

6. Je, Klinzy Barasa ameoa?

Haijabainika wazi ikiwa Barasa ameoa, lakini kuna picha mbili za wanawake tofauti kwenye mitandao yake.

Picha ya hivi karibuni ni ya mwaka 2021 ambapo anaonekana akizungumza kwa simu huku mwanamke akiwa anajipiga selfie pembeni yake.

Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi
Klinzy Barasa akiwa na sare ya polisi. Picha: Klinzy Barasa.
Chanzo: Instagram

7. Wakenya wanasema nini kuhusu Klinzy Barasa?

Uchunguzi wa haraka wa kurasa zake za mitandao ya kijamii unaonyesha maoni mengi kutoka kwa Wakenya.

Wengi walieleza hasira zao kuhusu hatua zake zinazodaiwa, wengine wakitumia lugha kali isiyochapishika.

Barasa na Kiprono kwa sasa wako mikononi mwa maafisa wa DCI wakisubiri hatua zaidi.

Klinzy Barasa Masinde: Picha 7 za Afande Anayedaiwa Kumpiga Risasi Muuza Barakoa Nairobi
Wakenya walifurika kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za Klinzy Barasa. Picha: Klinzy Barasa.
Chanzo: Instagram

Je, Boniface Mwangi Kariuki bado yuko hai?

Kariuki kwa sasa anapokea matibabu katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

Kwa mujibu wa madaktari, bado hajazinduka lakini ameonyesha dalili za kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura.

Ingawa kitu kilichoondolewa kichwani mwake kinahofiwa kuwa risasi ya mpira, wahudumu wa afya hawajathibitisha hilo na wameikabidhi kwa mamlaka husika kwa uchunguzi wa kitaalamu.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Francis Silva avatar

Francis Silva (Swahili translator) Francis M Silva ni Mkuu wa Kitengo cha Kiswahili. Ana tajriba ya miaka mingi katika taaluma ya uwanahabari hasa tafsiri, uhariri - Radio, TV na Dijitali. Yeye ni zao la Taasisi ya Mawasiliano-Umma ya Kenya (KIMC). Wasiliana naye kupitia: [email protected]

OSZAR »