Video ya Wakili wa Klinzy Barasa, Felix Kiprono, Akizungumza kwa Lafudhi Feki ya Kimarekani Yaibuka

Video ya Wakili wa Klinzy Barasa, Felix Kiprono, Akizungumza kwa Lafudhi Feki ya Kimarekani Yaibuka

  • Wakili wa Klinzy Barasa si mgeni kwa utata kwenye mitandao ya kijamii, kwani tayari jina lake liliwahi kupepea katika miaka ya hapo nyuma
  • Wakili huyo, Felix Kiprono, aliwahi kuvuma mwaka 2015 baada ya kutoa ombi la kipekee kwa Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama
  • Video hiyo iliyojitokeza tena imewaacha wengi wameshtuka, wakisema kuwa mtandao kamwe hausahau, na Wakenya daima watakumulika

Video ya zamani ya wakili wa Klinzy Barasa, Felix Kiprono, imeibuka ikimuonyesha miaka ya nyuma baada ya kupata umaarufu wa muda mfupi.

Video ya Wakili wa Klinzy Barasa, Felix Kiprono, Akizungumza kwa Lafudhi Feki ya Kimarekani Yaibuka
Picha ya Felix Kiprono wakili chipukizi (kushoto) na mwonekano wake wa sasa. Picha: Felix Kiprono, Sauti TV.
Chanzo: Instagram

Barasa ni afisa wa polisi anayekabiliwa na mashtaka ya kumpiga risasi Boniface Kariuki, mchuuzi, kichwani, na kwa sasa yuko rumande.

Afisa huyo wa polisi alimwajiri wakili Felix kumwakilisha, ambaye alijitokeza mbele ya vyombo vya habari akimtetea mteja wake kabla ya kesi kufikishwa mahakamani.

Alisisitiza kuwa mteja wake hana hatia na akadai kuwa madai hayo ni suala la utambulisho wa kimakosa.

Imebainika kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Felix kuingia kwenye vyombo vya habari.

Je, Felix Kiprono aliwahi kuonyesha nia ya kumuoa binti wa Obama?

Felix alipata umaarufu wa kimataifa mwaka 2015, baada ya kutoa posa ya ng’ombe 50, kondoo 70, na mbuzi 30 kwa ajili ya kumuoa Malia Obama, binti wa Barack Obama.

Wakili huyo alieleza kuwa mapenzi yake yalikuwa ya dhati na hakuwa akiwinda mali ya familia ya Obama, kinyume na kile ambacho watu wengi walikuwa wakifikiria.

Miaka 10 baadaye, video ya mahojiano yake na Joy Doreen kwenye KTN imeibuka tena.

Katika video hiyo, Felix aliongea kwa lafudhi ya Kiingereza ya Kimarekani, ambayo ilionekana kuwa ya kuiga kwani ilikuwa vigumu kuelewa alichokuwa akisema.

Doreen alitoa maoni kuhusu lafudhi hiyo, akisema ilikuwa karibu haiwezekani kumwelewa, lakini Felix alikana kuigiza lafudhi hiyo.

Alisema kuwa ndivyo alivyozungumza siku zote na hakuonekana kujali kuhusu ukosoaji huo.

Felix pia alisema kuwa pendekezo la posa halikutoka kwake binafsi, bali kutoka kwa jamii yake, na halikuwa kwa sababu Obama alikuwa akija Kenya wakati huo—jambo ambalo lilitokea kwa bahati tu.

Baadhi ya maoni kuhusu video hiyo ni kama ifuatavyo:

@Celestialchirp alisema:

"Hiyo lafudhi ni kitu gani kweli."

@Koganda_254 alisema:

"Ni lafudhi ya kifahari inayotambulika Uingereza."

@CMdamu1 alisema:

"Mtu wa aina hii anafaa kuwa mchekeshaji kwanza, halafu ahamie kuwa wakili. Kusomea sheria kama shahada ya kwanza ni ucheshi mtupu, ukiangalia video hizi mbili."

Nancie alisema:

"Makosa kidogo tu Kenya unakumbushwa enzi zako za uzee."

Alex Mwendwa alisema:

"Hii maisha, hata ujifiche aje, kuna mtu tu ana receipts zako za miaka 10 iliyopita."

Mercy mercie alisema:

"Sasa hapa ndipo msemo 'Internet haisahau' unapopatikana kwa ukamilifu."

@joymwikali22 alisema:

"Amejaa aibu jameni, OMG!"

Klinzy Barasa afuta ukurasa wake wa TikTok

Katika habari nyingine, Barasa anaonekana kufuta ukurasa wake wa TikTok kufuatia msukosuko uliotokana na tuhuma za kumpiga risasi Kariuki.

Afisa huyo alikuwa maarufu kwa kupakia video zake akiwa anasinkia midomo kwa nyimbo, kuonyesha mavazi yake ya kazi au kushiriki simulizi mbalimbali.

Hata hivyo, baada ya 'salamu' kutoka kwa wananchi walipoanza kumhusisha na tukio hilo la risasi, aliamua kuufuta ukurasa huo kabisa.

Mwanzoni, alikuwa amezuia maoni kwenye akaunti yake, lakini baada ya shinikizo kuongezeka, akaamua kuifuta kabisa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

Vichwa:
OSZAR »