Juma Jux Asema Hataki Kuwa na Baby Mamas: "Naomba Mwenyezi Mungu Sana"
- Juma Jux alisema ipo haja ya kujenga familia imara na kuepuka kujihusisha na mahusiano na baby mama tofauti
- Msanii huyo alieleza kuwa anatamani kupata watoto, lakini hana haraka ya kuwa mzazi, akisema ameacha yote kwa wakati wa Mungu
- Jux alifichua kuwa amejiwekea nia ya kujenga familia pamoja na mkewe Mnigeria, Priscilla Ajoke
Nyota wa muziki wa R&B kutoka Tanzania, Juma Jux, ambaye jina lake kamili ni Juma Mussa Mkambala, ni mtu anayependa familia na anaamini katika maadili ya kifamilia.

Chanzo: Instagram
Jux alizuru Kenya kwa ajili ya harusi ya kifahari ya Brian Belio, mwanawe Katibu Mkuu wa Uhamiaji Belio Kipsang, na Nicole Langat, binti ya bilionea David Langat.
Katika harusi hiyo, Jux alitoa burudani ya kipekee na hata akapata nafasi adimu ya kumtumbuiza Rais William Ruto.
Kwa nini Juma Jux hataki kuwa na baby mama
Jux, akiwa kwenye mahojiano na SPM Buzz, alifichua kuwa hataki kuwa na “baby mama” – yaani hataki kuzaa na mwanamke halafu wametengana.
Anasema anapenda kujenga familia imara na mke wake mrembo, Priscilla Ajoke, ambaye ni mrembo wa mitindo kutoka Nigeria.
“Sitaki kuwa na baby mamas tofauti. Hilo ni jambo ambalo humwomba Mungu sana. Hata kama nitakuwa na watoto wengi, nataka wawe na mama yao mmoja,” alisema.
Msanii huyo alieleza kuwa hawezi kudhibiti jinsi kila kitu inayokuwa, lakini anaamua kujikita katika kile anachoweza kufanya, huku akimuachia Mungu maamuzi mengine.
“Mimi nafanya, Yeye (Mungu) anaamua. Sijijazi mawazo. Lakini watoto wengi maana yake ni kazi nyingi... ila ni mpango wa Mungu. Na kila mtoto nitakayejaliwa atakuwa baraka,” aliongeza.
Alipoulizwa kama anahisi presha ya kupata watoto na Priscilla, Jux alisema anatamani kuwa na watoto, lakini haharakishi, akiamini kila kitu kitaenda sawa kwa wakati wake.
“Mara nyingi mwanaume akiharakisha mambo, hayaendi vizuri,” alisema kwa hekima.
Je, Jux alizaa na Vanessa Mdee?
Kumekuwa na madai kwamba Jux ana matatizo ya uzazi, hasa kwa sababu hakuwahi kupata mtoto na mchumba wake wa zamani, Vanessa Mdee, ambaye sasa yuko na msanii Rotimi.
Katika mahojiano ya awali, Jux alikanusha madai hayo na kusema kuwa hawakuzaa kwa sababu hawakuwa tayari, na si kwamba alikuwa na matatizo yoyote ya kiafya.
“Kila kitu kina mpango wake. Kipindi tulichokuwa wote, hatukuwa tayari. Huenda baadaye alihitaji mtoto lakini wakati huo hakuwa na mimi. Hata mimi nina mipango yangu. Siwezi kupata mtoto kwa sababu watu wanashinikiza,” alieleza.
Jux alisisitiza kuwa hadi sasa hajawahi kupata mtoto na mwanamke yeyote aliyewahi kuwa naye.
Jux alimzawadia nini Priscilla katika harusi ya pili?
Hapo awali, Jux alimzawadia Priscilla zawadi ya kifahari ya Range Rover Velar yenye thamani ya KSh 12 milioni.
Zawadi hiyo ilikamilisha sherehe yao ya harusi kwa mtindo wa kuvutia.
Priscilla alifurahia kiasi cha kutoa machozi ya furaha, akipiga mayowe na kukumbatiana kwa shukrani.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke