Nigeria: Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Ahukumiwa Kifo kwa Kumuua Mpenziwe

Nigeria: Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Ahukumiwa Kifo kwa Kumuua Mpenziwe

  • Mwimbaji wa nyimbo za injili amehukumiwa kifo kwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake
  • Msanii huyo alimkata vipande vipande mwanamke huyo wa miaka 24 ambaye walikuwa wamedumu katika uhusiano kwa mwaka mmoja, na alipatikana na kichwa chake
  • Mama na dada wa marehemu walizungumza na wanahabari baada ya hukumu na kusema kuwa haki imetendeka

Familia imepata afueni na kuridhika baada ya binti yao aliyeuawa kupata haki.

Nigeria: Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Ahukumiwa Kifo kwa Kumuua Mpenziwe
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Oluwatimileyin Ajayi (kulia) ahukumiwa kifo kwa kumkatakata mpenzi wake Salome. Picha: Alome Adaidu/ Caeser.T.
Chanzo: Instagram

Katika kesi hii, mwimbaji wa nyimbo za injili alipewa hukumu ya kifo kwa mauaji ya kikatili ya mpenzi wake.

Hukumu ilisomwa Alhamisi, Juni 25, ikiongozwa na Jaji Simon Aboki.

Mwimbaji huyo, Oluwatimileyin Ajayi, alipatikana na hatia ya kumuua Salome Adaidu, ambaye alikuwa mshiriki wa Huduma ya Taifa ya Vijana (NYSC).

Kulingana na Vanguard News, Ajayi pia alikata viungo vya mwili wa Adaidu katika hukumu iliyotolewa katika Mahakama Kuu ya Lafia, Jimbo la Nasarawa, Nigeria.

Polisi walimkamata mwimbaji huyo wa nyimbo za injili baada ya kupatikana na kichwa cha Salome kilichokatwa Jumapili, Januari 12, karibu na kanisa katika eneo la Orozo.

Video iliyosambaa mitandaoni ilimuonyesha Ajayi akihojiwa na watu waliokusanyika, ambapo alidai Salome alikuwa mpenzi wake na walikuwa wamechumbiana kwa takriban mwaka mmoja.

Hata hivyo, familia ya Salome ilikanusha madai hayo.

Kulingana na polisi, Ajayi anadaiwa kumuua Salome alipomtembelea nyumbani kwake katika eneo la Papalana, New Karshi, katika Kaunti Ndogo ya Karu, Jimbo la Nasarawa.

Ajayi alipatikana na silaha zinazodhaniwa alizotumia kutekeleza uhalifu huo, zikiwemo kisu na mapanga.

Nigeria: Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Ahukumiwa Kifo kwa Kumuua Mpenziwe
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Ajayi alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Salome. Picha: James Alba / X.
Chanzo: Twitter

Familia ya Salome yaeleza hisia zao baada ya hukumu

Patience Unekwuojo, mmoja wa wanafamilia, alizungumza na BBC Pidgin baada ya hukumu hiyo ya mahakama.

Alieleza kuwa ingawa hakuna kilichoweza kumrudisha dada yake, alihisi kuwa haki imetendeka.

Alisema kuwa Mungu ndiye anayesimamia kila kitu.

Aliongeza kuwa Salome alikuwa na mipango mikubwa ya baadaye, ikiwemo kozi ya kitaaluma aliyokuwa ameanza katika kampuni ya bima ya Nicon. Salome alikuwa na umri wa miaka 24.

Mama yake Salome pia alieleza huzuni yake, akisema kuwa alimchukulia Salome kama mumewe aliyefariki, na akaahidi kutafuta haki kwa ajili ya binti yake.

Jinsi kesi ya Ajayi ilivyoendelea

Baada ya Ajayi kukamatwa kama mshukiwa mkuu wa mauaji ya Salome, kesi iliwasilishwa mahakamani.

Familia ya Adaidu ilitaka haki itendeke walipokuwa wakimlilia binti yao kwa huzuni.

Mahakama ilianza kusikiliza kesi hiyo, huku jaji akisisitiza kuwa kesi hiyo isikilizwe kwa haraka kutokana na umuhimu wake kwa taifa.

Ajayi alikana mashtaka yote. Kesi iliendelea hadi Machi 2025, na tarehe ya kusikilizwa ilipangwa kuwa kati ya Machi 17 hadi 20, 2025.

Hukumu ya mwisho ilimpa Ajayi adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Watu walivyoreact baada ya Ajayi kuhukumiwa kifo

Baada ya hukumu hiyo, wengi walieleza kuridhika kwao, wakisema kuwa haki hatimaye imetendeka, jambo lililowafariji familia ya Salome.

Maoni ya watu:

Prince Ugo: "Haki imetendeka, lakini ni kumbusho chungu kuhusu jinsi uovu unaweza kuwa mkubwa. Roho ya Salome ipumzike kwa amani. Huu uwe ujumbe mzito – hakuna aliye juu ya sheria."

Paul Udechime: "Alisema hana majuto kumuua Salome, basi hata kunyongwa hatasikitika."

Obijiaku Chika Chycosy: "Ndivyo walivyomhukumu mume wa Osinachi lakini hawakuonesha utekelezaji 😔."

Oreofefabrics: "Haki imetendeka! Safari njema, mpendwa Salome 😥😢."

Nkechi April: "Asante Mungu 🙌🙌🙌🙌."

Lizzy Joel: "Nimefurahia sana hukumu hii – auae na yeye atauawa. Anastahili hukumu hiyo."

Akua Darkowaa Mensah: "Haki imetendeka 👏."

P Patience Danjuma: "Auae kwa upanga 🗡️⚔️ atauawa kwa upanga. RIP."

Moses Ohaba: "Ni funzo kwa wale walio na nia mbaya katika jamii yetu leo."

Vincent Banger: "Anastahili hiyo hukumu."

Calvert Amaka: "Hukumu nzuri!"

Jowie Irungu pia ahukumiwa kunyongwa

Katika taarifa nyingine, Mkenya Joseph Irungu almaarufu Jowie alihukumiwa kifo.

Jaji Grace Nzioka alitangaza hukumu hiyo Machi 13, 2024, kufuatia kutiwa hatiani Februari 9, 2024, kwa mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani mnamo Septemba 2018.

Ingawa mauaji kwa kawaida hupewa adhabu ya kifo nchini Kenya, uamuzi wa awali wa mahakama uliondoa adhabu hiyo kuwa ya lazima.

Hata hivyo, Jaji Nzioka alikiri kuwa katika baadhi ya kesi maalum, hukumu ya kifo bado inaweza kuonekana kuwa ya haki, licha ya kupingwa kwa jumla.

Jaji alimhukumu Jowie kifungo cha kunyongwa kwa makosa matatu, akifutilia mbali uwezekano wa adhabu isiyo ya kifungo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »