Babake Albert Ojwang' kwa Uchungu Awaachia Ujumbe Mzito Waliomuua Mwanawe: “Hawatakuwa na Amani"

Babake Albert Ojwang' kwa Uchungu Awaachia Ujumbe Mzito Waliomuua Mwanawe: “Hawatakuwa na Amani"

  • Kanisa la Ridgeways Baptist lililoko Barabara ya Kiambu liligubikwa na huzuni Julai 2 huku waombolezaji wakikusanyika kwa ibada ya heshima ya mwisho ya bloga aliyeuawa, Albert Ojwang
  • Meshack Opiyo, babake Albert, alitoa ujumbe wa kutisha uliotokana na Maandiko Matakatifu, akionya wauaji wa mwanawe kwamba damu waliyoimwaga itakuwafuata
  • Wakenya walifurika mitandaoni na jumbe za huzuni, wakisimama pamoja na familia inayohuzunika na kurudia miito ya kutaka haki itendeke

Babake bloga aliyeuawa, Albert Ojwang, Meshack Opiyo, alitoa ujumbe mzito wakati wa ibada ya wafu iliyojaa majonzi siku ya Jumanne, Julai 2, katika Kanisa la Ridgeways Baptist.

Babake Albert Ojwang Atuma Ujumbe wa Maumivu kwa Wauaji wa Mwanawe: “Hawatakuwa na Amani”
Baba yake Albert Ojwang alinukuu maandiko matakatifu alipotoa ujumbe mzito kwa wauaji wa mwanawe. Picha: Mutembei TV, Albert Ojwang.
Chanzo: Youtube

Mzee huyo alitoa ujumbe mzito uliojaa maonyo ya kiroho kwa wale waliohusika na mauaji ya kikatili ya mwanawe.

Meshack aliwaambia nini wauaji wa Ojwang’?

Baba huyo aliyekuwa akihuzunika alisimama mbele ya waumini waliokuwa wakilia na kunukuu Maandiko Matakatifu alipowahutubia waliomuua mwanawe.

Akinukuu kutoka kitabu cha Mithali sura ya 21 na hadithi ya bibilia ya Kaini na Abeli, aliwakumbusha waombolezaji kuwa damu isiyo na hatia haikomi kulilia haki.

“Kulingana na tafsiri yangu, damu ni ya kiishara. Haifi, na inaweza kuleta uchungu na mateso,” Meshack alisema kwa huzuni.

Aliendelea:

“Damu inayomwagika ardhini bila sababu ya haki huleta uchungu na mateso.”

Ujumbe wa Meshack ulilenga moja kwa moja kwa wauaji wa mwanawe, ambao vitendo vyao vimezua hasira kote nchini na wito wa haki kutendeka.

Aliwalaumu kwa ukatili wao na akaonya kuwa haijalishi jinsi wanavyojaribu kuficha uhalifu wao au kujipamba hadharani, kamwe hawatapumzika kwa amani.

“Nataka niseme kwamba damu hiyo ya Albert ambayo imemwagika bila hatia, waliochukua maisha ya mwenzao na kumwaga damu na kuficha uovu wao, watabaki na heshima, utajiri na sifa za aina yoyote lakini hawatakuwa na amani,” alitangaza.

Ojwang’ alifariki kwa njia ya kutatanisha akiwa mikononi mwa polisi, jambo ambalo liliwasha hasira miongoni mwa Wakenya.

Tazama baadhi ya maoni ya watumiaji wa mitandao ya kijamii:

Dessah Debrah:

“Anajua uchungu zaidi ya mtu mwingine yeyote.... uchungu wa mwana.”

Boss Malawi:

*“Maneno haya yanafanana na yale ya Babake Adika aliposema 'na wafe kama alivyokufa Adika' katika tamthilia ya Betrayal in the City.”

Juliet Wacike:

“Mzee nina mengi ya kukuambia lakini kwa sasa pokea rambirambi zangu za dhati.”

Karen Kasyoka Muasya:

“Wacha damu ya Albert inene kama vile damu ya Abeli ilinena kwa Kaini.”

Ma Abujubuju:

“Nilisema awali itamgonga baba kwa uchungu wakati atamwona Albert akizikwa. Mungu aitie nguvu familia hii.”

Debra Awino:

“Kisasi ni cha Bwana.”

Virginia Muthoki:

“Albert alipitia mateso hadi kufa wakati baba yake alikuwa safarini usiku kucha kujaribu kumuokoa kwa hati miliki. Mungu asiwape pumziko waliomuua.”

Jane Akeyo:

“Mungu alinde na afunike familia nzima kwa damu ya Yesu Kristo. Lala salama Albert.”

Joel Tsanze:

“Rambirambi zangu za dhati kwa familia. Kisasi ni cha Bwana. Lala salama ndugu hadi ile asubuhi ya kung'aa. Amina.”

Maneno ya mwisho ya Ojwang’ kwa mkewe kabla ya kifo ni yapi?

Wakati wa ibada hiyo hiyo, mjane wa Ojwang’, Nevnina, alilemewa na hisia alipoelezea maneno ya mwisho ya mumewe.

Alisema yeye ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuzungumza na marehemu akiwa mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Central.

Kulingana naye, Ojwang’ alimwambia kuwa anampenda na kwamba wangekutana hivi karibuni, bila kujua kuwa mkutano huo ungekuwa mochari.

Licha ya maumivu, alieleza azimio lake la kubaki imara kwa ajili ya mtoto wao na akaonesha upendo wake wa dhati kwa marehemu mumewe.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

Vichwa:
OSZAR »