Familia ya Albert Ojwang Yakanusha Madai ya Eric Omondi Kupokea KSh10m ya Michango
- Mchekeshaji aliyegeuka kuwa mwanaharakati Eric Omondi alidai kuwa wakfu wake wa hisani ulichangisha takriban KSh 10 milioni kwa ajili ya familia ya Albert Ojwang
- Wakili wa familia hiyo alirekebisha rekodi hiyo, na kufichua uchanganuzi wa kina wa michango ambayo walipokea
- Wakenya walimiminika haraka mitandaoni wakitoa hisia miseto wengine wakimtetea Eric vikali, huku wengine wakisifu familia hiyo kwa uaminifu na uwajibikaji wao
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Familia ya mwanablogu aliyeuawa Albert Ojwang imejitokeza kuweka sawa rekodi kuhusu kiasi cha pesa ambacho wamepokea kutokana na michango kufuatia kifo cha mwana wao.

Chanzo: Youtube
Wakati wa misa ya wafu iliyoandaliwa siku ya Jumanne, Julai 2, katika Kanisa la Ridgeways Baptist jijini Nairobi, wakili wa familia hiyo, Julius Juma, alihutubia waombelezaji, na kufafanua kile alichotaja kuwa habari potofu zilizoenea kuhusu msaada waliopokea.
Familia ya Ojwang ilipokea pesa ngapi?
Kauli yake inajiri baada ya madai yaliyotolewa na mchekeshaji aliyegeuka kuwa mwanaharakati Eric Omondi, aliyedai kuwa wakfu wake wa Sisi kwa Sisi ulisaidia kuchangisha takriban KSh 10 milioni kwa familia ya Ojwang.
"Imesemwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwamba familia ilipokea KSh 10 milioni. Nimeombwa kuweka rekodi sawa, na ninafanya hivyo kutoka kwenye mimbari, nikifahamu kikamilifu matokeo ya kusema uwongo," wakili alisema.
Aliendelea: "Familia hiyo haikupokea KSh 10 milioni. Familia inataka kuthibitisha kwamba ilipokea KSh 2 milioni kutoka kwa Mkuu wa Nchi, KSh 1 milioni kutoka kwa Raila Odinga, na KSh 2 milioni kutoka kwa Wakenya waliochangia pesa mbalimbali. Jumla hizi zote zilifikia KSh 5,060,000. Narudia, si kweli kwamba familia ilipokea KSh milioni 10."
Wakenya walisema nini kuhusu michango ya mazishi ya Ojwang?
Ufichuzi wa familia hiyo uliwaacha Wakenya wakiwa wamegawanyika. Ifuatayo ni baadhi ya maoni kutoka kwa wanamitandao.
Cynthia Wanza: "Naamini Eric, kesi imefungwa."
Muli Tim: "Lakini wanapaswa kumshukuru, yeye ndiye aliyekuja na wazo hilo."
Edith Mucheywa: "Chochote walichopata, wacha waweke bajeti kwa ajili hiyo, kwani walikuwa wapate wapi, tujifunze kuthamini kidogo tulichonacho."
Malesi Cathrine Isinga: "Kitu cha bure hata kama ni ten bob shukuru,alikua anapata wapi?Asitusumbulie Erick Omondi akili.RIP Albert."
Lydiah Moindi: "Vipi kuhusu ahadi ambayo Bw Dimples aliwapa?"
Ngungi Kanui: "Watu wanapaswa kujifunza kuthamini chochote wanachopata."
Anne Wangu: "Familia ina haki ya kushiriki kuhusu michango kwa madhumuni ya uwajibikaji." Jully Mash: "Erick Omondi, you are a great person. Sioni any body of influence anaeza kusaidia kuraise kiasi hicho..
Nyambuh Maureen: "Pesa zilikua zinaingia kwa mstari wa Mzee..hapo Eric anaingilia wapi?" Philo Protich: "Na hazina hiyo inasemaje?...au Eric Omondi ndiye hazina ya familia?"
Isac Cerony: "Ikiwa uko mbele kufadhili kila wakati, utakosea kwa kuwa na nia mbaya ndani yake!"
Lilian Sotian: "Kwa nini watu hawasikii... .kulingana na taarifa ni kwa madhumuni ya uwazi sio haki. Ni vizuri kuona mambo zaidi ya masuala yako ya hasira."

Chanzo: Twitter
Babake Ojwang aliwaambia nini wauaji wake?
Wakati wa misa hiyo hiyo, babake Ojwang, Meshack Opiyo, alituma onyo kali kwa wauaji wa mwanawe.
Alisoma Biblia na kutafakari jinsi kumwaga damu isiyo na hatia kunavyoleta maumivu na kuteseka.
Kisha Meshack akatangaza kuwa wahusika wa mauaji ya mwanawe hawatawahi kuwa na amani kamwe.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke