Boniface Kariuki: Huzuni Eric Omondi Akiwaongoza Watu Kuvaa Maski kwa Heshima ya Mchuuzi Aliyeuwawa

Boniface Kariuki: Huzuni Eric Omondi Akiwaongoza Watu Kuvaa Maski kwa Heshima ya Mchuuzi Aliyeuwawa

  • Waombolezaji katika Kanisa la All Saints Cathedral walionekana kushtushwa baada ya ishara ya kipekee kutoka kwa Eric Omondi kuwakumbusha kile ambacho Boniface Kariuki alikuwa akiuza wakati wa tukio la kusikitisha
  • Hotuba yenye nguvu ya Eric iliwavutia wengi alipomkosoa moja kwa moja Rais William Ruto kuhusu agizo lake la "kupiga kwa kujeruhi"
  • Mchekeshaji huyo pia alitoa tamko la kuthubutu kuhusu hali ya sasa nchini, akiwataka viongozi wa kidini kuiombea taifa

Eric Omondi, mchekeshaji aliyebadilika kuwa mwanaharakati, kwa mara nyingine aliwagusa Wakenya kwa hisia wakati wa heshima za mwisho kwa Boniface Kariuki.

Boniface Kariuki: Huzuni Eric Omondi Akiwaongoza Watu Kuvaa Maski kwa Heshima ya Mchuuzi Aliyeuwawa
Boniface Kariuki alipigwa risasi kichwani na polisi wakati wa maandamano. Picha: SPM.
Chanzo: Instagram

Kariuki ndiye mchuuzi aliyepigwa risasi kichwani kwa karibu na polisi wakati wa maandamano dhidi ya ukatili wa polisi jijini Nairobi.

Eric Omondi alisema nini katika ibada ya kumuombea Kariuki?

Ibada ya kihisia ya kumuombea marehemu Kariuki, iliyofanyika Julai 9 katika Kanisa la All Saints Cathedral, ilihudhuriwa na familia ya karibu, marafiki na waombolezaji waliofika kuenzi maisha ya kijana huyo mchuuzi wa barakoa.

Eric, ambaye amekuwa akiiunga mkono familia hiyo tangu wakati Kariuki alipopigwa risasi hadi kufariki kwake, alitoa hotuba ya rambirambi iliyojaa huzuni, hasira na wito wa haki.

Katika ujumbe wake, alilaani agizo tata la Rais William Ruto la kuwafyatulia risasi waandamanaji kwa lengo la kuwajeruhi, akionya kwamba sera kama hizo zinaweka maisha ya watu wasio na hatia hatarini.

“Nataka kusema pole kwa mzee na mama. Nawaomba kanisa mtuombee kama taifa, kuna kitu hakiko sawa. Amesema wapige kwa mguu… tunahitaji maombi, kwa sababu rais anapowaambia maafisa wa usalama wapige raia, katika vurugu hizo huwezi kujua. Tuache kutumia risasi – iwe ni risasi halisi au za mpira,” alisema kwa uchungu.

Mchekeshaji huyo pia alikumbuka jinsi alivyoiomba serikali kutumia tukio la kupigwa risasi kwa Kariuki kama mwisho wa ukatili wa polisi kupitia maandamano yake ya kimya aliyoyaita Mask Friday.

Hata hivyo, siku chache baadaye, msichana wa miaka 12 na wengine kadhaa waliuawa wakati wa maandamano ya Saba Saba yaliyogeuka vurugu.

Waombolezaji walimuenzi vipi Kariuki?

Katika tukio la kihisia lenye ishara kubwa, Omondi alisambaza barakoa kwa waombolezaji na kuwaomba wazivae kumkumbuka Kariuki, kwani zilikuwa sawa na zile alizokuwa akiuza alipopigwa risasi.

“Nataka tuchukue dakika moja ya kimya kumuenzi ndugu yetu. Vaa hiyo mask kwa sababu hii ndiyo alikuwa anauza,” aliwaambia waumini waliokuwa kimya kanisani.

Omondi alihitimisha hotuba yake kwa tamko lenye matumaini makubwa, akiwambia waombolezaji kuwa harakati zinazoendelea ni sehemu ya mabadiliko makubwa nchini.

“Wakati wa Kenya mpya umefika. Endeleeni kupigania, tutafika,” alisema kwa msisitizo.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii:

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »