Rongai: Makanga Roho Safi Afunguka Makubwa Baba Mtoto wa Yule Mwanamke Aliyesaidia Anamchamba Mbaya
- Telvin Mburu, utingo aliyemwokoa Viola Nekesa ndani ya matatu, alishangazwa na jumbe kutoka kwa baba ya mtoto wa Viola
- Anasema hamkosei mtu huyo, lakini anahisi huenda anadhani wana uhusiano wa kimapenzi na Viola, ambaye alipoteza kazi hivi karibuni.
- Telvin alikanusha madai hayo, akisema hana uhusiano naye na bado anahangaika kifedha
- Ameanza kujikomboa kwa kupata leseni ya udereva kama hatua ya kuelekea uthabiti
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Rongai: Telvin Mburu, utingo wa zamani wa Rongai ambaye alisifiwa kwa kumwokoa mwanamke aliyejulikana kama Viola Nekesa, amefichua kuwa baba wa mtoto wa Viola alimpigia simu na hata kutuma jumbe akihusiana naye.

Chanzo: Facebook
Je, Telvin alitishwa?
Kupitia mfululizo wa jumbe kwenye TikTok, utingo huyo kijana alisema kuwa mwanaume huyo aliendelea kumtumia ujumbe na hata kufichua sababu ya kumuacha Nekesa.
"Mimi ni Eugene, baba wa mtoto wa Viola; unafikiri hivyo vitu vya TV na redio vitakusaidia? Nilimuacha kwa sababu ya tabia zake kazini," alisema.
TUKO.co.ke walipomfikia Telvin, kijana huyo alisema jumbe zilianza kumjia baada ya kumwokoa Nekesa lakini Eugene hakumtishia wala kuhatarisha maisha yake kwa njia yoyote ile.
"Sijui kilichomsababisha aanze kunitumia jumbe; nahisi baba wa mtoto anadhani nina uhusiano naye," alisema Telvin.
"Mimi na Viola hatuna uhusiano wa kimapenzi, sijui kwanini amechukizwa. Kwa sasa siwezi kuingia katika uhusiano kwani sijajitegemea. Wakenya walinishauri nipate leseni ya udereva ili nianze kazi, na hiyo ndiyo hatua ya kwanza niliyopiga kuelekea uhuru wa kifedha," aliongeza.

Chanzo: Facebook
Viola anasemaje kuhusu jumbe hizo?
TUKO.co.ke walipomfikia Viola, mama wa watoto wawili alikiri kuwa alisikia taarifa hizo baada ya Telvin kuzichapisha na kumshirikisha.
"Ndiyo, alinikabili kwa kunisababisha nisimamishwe na polisi lakini suala hilo halikupata suluhu," alisema.
"Baba wa mtoto alikuwa na hasira kama kawaida ya wazazi wasiohusika... hawana furaha wanapoona unapiga hatua bila msaada wao. Kwa ukweli, sitaki hata aitwe baba wa mtoto kwani hajawahi kuwa hivyo," aliongeza.
Wakenya wanasemaje kuhusu tukio hili?
Lisa: "🤣🤣🤣 Kama alikuwa mbaya, kwa nini bado anamfuatilia?"
Lilibeth: "Wanaume si mkienda tu muende na muache wivu, kama haikufanya kazi wakati huo si ati itafanya sasa."
Salha Mamake: "Mwambie kwa sababu alikuwa mbaya anafaa kumsahau kabisa, hata jina lake asilitaje. Kwanini anamfuatilia na ilhali ni mbaya? Wivuuu."
Gal dem...💋: "Mimi hushindwa na wanaume... ukiwa naye anakudharau, ukitoka ndio anagundua ulikuwa wa maana... ukiona hivyo."
angieangiemesh: "Wee ex wa Viola ana wivu tu... aliwaacha, si aendelee na maisha yake aache Viola apumue. Wivu wa wanaume wengine... Mungu awafungulie milango ya baraka hadi maadui waone aibu."
yummy and delicious: "Ongeza sauti tafadhali... ukiona analalama ujue alipoteza dhahabu."
gsggsygi: "Kuna zamani na sasa, aende akiendaga ni wewe sasa rais 😅😅."
@lilybet: "Waaah, natarajia aende kumshtaki huyo dem apoteze kazi. Saitan. Wivu utamuua 🤣."
Viola Nekesa anakabiliwa na hatari ya kufukuzwa
Katika habari nyingine, Nekesa ambaye alienea sana mtandaoni baada ya kuokolewa ndani ya matatu, alifichua kuwa sasa anakabiliwa na kufukuzwa baada ya mwenye nyumba anayoishi kukata maji na umeme.
Licha ya kupata huruma kutoka kwa umma, alieleza kuwa watu wengi waliamini kupoteza kazi kwake kulikuwa maigizo, lakini ilikuwa kweli.
Nekesa ni mama mzuri wa watoto wawili wadogo na amekuwa akiwaangalia mwenyewe. Amewaomba watu wenye nia njema kumsaidia apate kazi au dili la kuwa balozi wa chapa ili aweze kuishi.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke