Nairobi: Nyanya Akwama Baada ya Simu Yake Kuibwa Akielekea kwa Nduguye

Nairobi: Nyanya Akwama Baada ya Simu Yake Kuibwa Akielekea kwa Nduguye

  • Bibi mwenye umri wa miaka 70, ambaye alikuwa amepanga kumtembelea kakake jijini Nairobi amekwama baada ya mtu kumpokonya simu yake CBD
  • Wasamaria wema walimsaidia kufika Ruai, lakini alishindwa kupata nyumba ya kaka yake kwa sababu mahali hapo pamebadilika tangu ziara yake ya mwisho
  • Msamaria Mwema alimpatia chakula na vinywaji kabla ya kumkabidhi katika Kituo cha Polisi cha Ruai, ambako ndiko aliko kwa sasa

Nairobi – Bibi mwenye umri wa miaka 70, amekwama baada ya simu yake kuibwa katika katikati ya jiji la Nairobi (CBD).

shosho
Nairobi: Bibi Alikwama Ruai Baada ya Simu Yake Kubiwa CBD Akiwa Amemtembelea Nduguye.
Chanzo: UGC

Mwanamke huyo mzee aliyetambulika kwa jina Lucy Wanjiku Wambugu alikuwa amesafiri hadi jijini kumtembelea kakake Mwangi Wambugu, anayeishi Ruai, lakini sasa hawezi kuwasiliana naye.

Je, Bibi Wanjiku alipotezaje simu?

Msamaria mwema Nancy Mburu aliiambia TUKO.co.ke kuwa simu ya nyanya huyo iliibwa CBD, na hivyo kukata njia yake pekee ya mawasiliano na urambazaji.

Alisaidiwa na watu wasamaria wema ambao walimpandisha kwenye matatu iliyokuwa ikielekea Ruai, wakitumaini kwamba angepata maelekezo pindi atakaposhuka.

Hata hivyo, alipofika Ruai, mwanamke huyo aligundua kuwa eneo hilo lilikuwa limebadilika sana tangu ziara yake ya mwisho, na kumwacha akiwa amechanganyikiwa.

Alimwendea Nancy katika eneo lake la kazi karibu na jukwaa la Ruai Quickmart kwa usaidizi wa kutafuta njia ya kufika kwa kaka yake.

"Alitoa maelezo mazuri ya nyumba ya kaka yake, na waendesha bodaboda walijaribu kufuatilia alama alizotaja," Nancy aliongeza.

Wanjiku yuko wapi sasa?

Wananchi ambao wanaweza kumtambua mwanamke huyo au kumfahamu kakake Mwangi Wambugu wamehimizwa kuwasiliana mara moja.

Kitambulisho cha mwanamke aliyepotea kinaonyesha alizaliwa Nyeri ya Kati mnamo Januari 1955, lakini hati hiyo ilitolewa Kiamaina.

Yeyote aliye na taarifa muhimu anaombwa kupiga simu 0706225055.

"Nilimnunulia godoro, na sasa analala katika chumba cha watoto waliopotea katika Kituo cha Polisi cha Ruai. Ninaelekea huko sasa kumpelekea kifungua kinywa," Nancy alisema.

nyanya
Nyanya Lucy Wanjiku Wambugu. Picha: Nancy Mburu.
Chanzo: UGC

Mwanamume aliyetoweka Dagoretti apatikana akiwa salama baada ya kutafutwa kwa wiki nzima

Katika hadithi yenye mwisho mwema, familia ya Alex Njoroge Kabiti ilipumua kwa ahueni wakati mfanyabiashara huyo wa Dagoretti aliporejea nyumbani baada ya kutoweka kwa takriban wiki moja.

Baba huyo wa mtoto mmoja alitoweka baada ya kumpeleka mkewe mtarajiwa katika Hospitali ya Kikuyu, na kusababisha msako mkali.

Jamaa walikuwa na wakati mgumu kuwasiliana naye kwani aliiacha simu yake.

Maelezo yanaonesha kuwa Alex aliingia kitandani moja kwa moja aliporudi lakini hakutoa maelezo ya mahali alipokuwa kwa siku sita alizokuwa ametoweka.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »