Uasin Gishu: Jamaa Aliyetoweka Siku 9 Zilizopita Apatikana Amefariki Karibu na Mto Sosiani
- Edwin Kiplimo Samoei alionekana mara ya mwisho siku ya Jumanne, Mei 27, jioni karibu na Shule ya Testimony huko Eldoret
- Habari za kupotea kwake zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku marafiki na familia wakianza kumtafuta
- Baada ya siku tisa za kumsaka, maiti yake imepatikana karibu na Simat, imetupwa kando ya Mto Sosiani
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Eldoret - Mwili wa Edwin Kiplimo Samoei, ambaye aliripotiwa kutoweka siku kadhaa zilizopita, umepatikana karibu na Simat, ukiwa umetupwa kando ya Mto Sosiani katika hali isiyoeleweka.

Chanzo: Facebook
Kiplimo, mkazi wa Kapsumbeiywet Farm huko Soy, alionekana mara ya mwisho jioni ya Jumanne, Mei 27, 2025, mwendo wa saa 8.30 usiku karibu na Shule ya Testimony jijini Eldoret.
Kalenjins Online iliripoti kwamba alikuwa amevalia kofia nyekundu, t-shirt nyeupe, na suruali ya beige siku ya kutoweka kwake.
Wanafamilia walikuwa wameanzisha msako mkali wa kumtafuta kijana huyo mwenye umri wa miaka 29, baada ya kushindwa kurejea nyumbani jioni hiyo.
Kutoweka kwake kulizua wasiwasi katika jamii, huku picha zake zikisambazwa katika mitandao ya kijamii kufuatilia aliko.
Cha kusikitisha ni kwamba matumaini yalikatizwa mapema leo wakati wenyeji walipogundua maiti yake karibu na Simat.
Mamlaka ya usalama ilifika katika eneo la tukio na kuzingira eneo hilo huku uchunguzi ukiendelea.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi.
Polisi wanamtaka yeyote aliye na habari kuhusu hatua za mwisho za Kiplimo usiku wa kupotea kwake kujitokeza.
Tukio hili linaongeza wasiwasi kuhusu visa vya watu waliopotea nchini, ambao wengi wao hupatikana wakiwa wameuawa.
Wakaazi na Wakenya kwa ujumla wanataka hatua bora za usalama na mwitikio wa haraka kutoka kwa mamlaka katika visa kama hivyo.
Mume wa mrembo wa Nakuru M-Pesa ahusishwa na mauaji yake
Huko jijini Nakuru, kesi inayohusu kutoweka kwa Hannah Wangare na kupatikana ameuawa ilichukua mkondo mpya baada ya mumewe kuhusishwa.
Wangare, mhudumu wa M-Pesa jijini Nakuru, alitoweka alipokuwa akielekea benki kuweka KSh 250,000 za mwajiri wake.
Baada ya kupekuliwa kwa siku kadhaa, maiti yake ilipatikana ikiwa imetupwa kwenye kinamasi, huku wachunguzi wakimtuhumu mumewe, Zachariah Wambugu Wanjohi, kwa mauaji hayo.
Afisa anayechunguza kesi hiyo aliambia mahakama kwamba ishara kutoka kwa nambari ya simu ya mumewe iligunduliwa ambapo ishara ya mwisho ya simu ya marehemu ilikuwa.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke