Video ya Money Bior Akiwagawa Pesa Wakazi wa Kasipul Akifanya Kampeni Yazua Gumzo Mitandaoni
- Money Bior ndiye mkazi wa hivi punde wa eneo bunge la Kasipul kutangaza wazi nia ya kugombea kiti cha ubunge kufuatia kifo cha Ong'ondo Were
- Alinaswa kwenye video akigawa mabunda ya noti kwa wakazi waliokuwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza akieleza sera zake
- Were, ambaye alikuwa Mbunge wa Kasipul, alipigwa risasi na kuuawa mnamo Aprili 30 katika barabara ya Ngong, na chama cha ODM kinadaiwa kumuidhinisha mmoja wa wanawe kuchukua nafasi yake
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Robert Ajwang, anayejulikana sana kama Money Bior, ameanza rasmi kampeni zake huko Kasipul katika juhudi za kumrithi marehemu mbunge Ong'ondo Were.

Chanzo: TikTok
Kifo cha Were kimewaweka watu wengi kwenye jukwaa la kisiasa, wote wakitumaini kuchukua uongozi wa eneo bunge la Kasipul
Bior ni miongoni mwa watu waliotangaza hadharani nia ya kuwania kiti hicho kama mgombea huru.
Akitambulika kwa mtindo wake wa maisha wa kifahari, Bior alishiriki video kwenye ukurasa wake wa TikTok akiwapa pesa wakazi waliokuwa wamepanga foleni ili kumuona.
Video hiyo inaanza na Bior akizungumza na kundi la vijana kabla ya kuwaomba wapange mstari ili kila mmoja apate pesa.
Kuna mstari mwingine ulikuwa na wanawake, baadhi wakiwa wamebeba watoto waliokuwa wakinyosha mikono yao kupokea pesa kabla ya kuondoka.
Ingawa kampeni za aina hii zimezoeleka katika maeneo mengi ya Nyanza, watu wengi wameikosoa vikali kwa kuchochea uongozi mbaya unaotokana na kura za kuhongana.
Aliandika kwenye ukurasa wake wa TikTok: "Mwanzo mpya kwa Kasipul unaanzia hapa. Pamoja tujenge, tukue na tuongoze."
Tazama baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii:
@12_becks: "Natumai siku moja wananchi wa nchi yangu wataokolewa kutoka kwa siasa za aina hii."
@David Jamba: "Huo ndio mwanzo mpya? Kuwapa watu mia moja?"
@Harry Smith: "Kuna vitu unafaa kuachia wengine. Tayari una pesa, sasa unataka kazi ya ubunge ya nini?"
@bimmertraveller: "Badala ya kutoa hela ndogo ndogo, kwanini usiendelee kuendeleza maendeleo ya eneo hilo?"
@Derrick Aseka: "Hiyo ndio unaita mwanzo mpya, kununua kura?"
@Eric Kinyua: "Watu waepuke kiongozi anayegawa pesa huku akirekodiwa na vyombo vya habari. Ni ishara ya hatari, mtalia mkimchagua mtu kama huyu."
Chama cha ODM chamtaka Raila amuidhinishe mwana Were
Katika taarifa nyingine, wakati wa mazishi ya Were, wengi wa wanachama wa ODM walimtaka mwanasiasa mkongwe Raila Odinga kumuidhinisha mwana wa marehemu, Boyd Were.
Wengi walieleza kuwa Boyd, ambaye ni mwana wa pili wa marehemu, ana uwezo wa kuendeleza kazi ya baba yake.
Alivutia hisia za waombolezaji waliofika kwao kwa ajili ya kumpa baba yake heshima za mwisho, alipoeleza kwa ujasiri haja ya kutendewa haki.
Kulikuwa na kicheko kidogo wakati Mwakilishi wa Wanawake wa Lamu alipomwomba Raila kumpeleka Boyd bungeni “ili apate mume.”
Kadri vita vya uongozi vinavyoendelea, wakaazi wa Kasipul wamegawanyika kuhusu nani wa kumchagua, kwani kila mgombea ana ufuasi mkubwa katika jamii.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke