Pasta Ng'ang'a Aijibu kwa Kiburi Serikali ya Kaunti Kuhusu Deni la Kodi ya Ardhi: "Sijakataa"
- Maafisa wa Kaunti ya Nairobi walitembelea kanisa la Mtume James Ng’ang’a ili kuwasilisha notisi kuhusu deni la KSh milioni 10 la ada ya ardhi linalohusishwa na mali ya kanisa lake
- Ng’ang’a alikana kukataa kulipa deni hilo, akieleza kuwa suala hilo liko mahakamani kwa sasa na akitaja msamaha wa awali kutoka kwa serikali
- Mchungaji huyo alitoa onyo kali kwa serikali ya kaunti, akipuuza hatua zao za hivi karibuni na kuonyesha imani yake katika mchakato wa kisheria unaoendelea
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Mtume James Ng’ang’a wa Neno Evangelism Centre amejibu vikali kufuatia ziara ya maafisa wa Kaunti ya Jiji la Nairobi katika kanisa lake wakidai deni la ardhi ambalo halijalipwa.

Chanzo: Facebook
Ng’ang’a alisema nini kuhusu deni la kodi ya ardhi?
Mnamo Mei 18, maafisa kutoka serikali ya kaunti wakiongozwa na Afisa Mkuu wa Mazingira Geoffrey Mosiria, walitembelea kanisa la Ng’ang’a ili kuwasilisha notisi kuhusu deni la KSh milioni 10 la ada ya ardhi ambalo linadaiwa Kaunti ya Nairobi.
Utata huo ulizuka baada ya kuripotiwa kuwa Ng’ang’a alidharau deni hilo akilieleza kuwa ni “takataka,” jambo lililosababisha maafisa wa kaunti kuchukua hatua kali.
Katika majibu ya hasira, Mtume Ng’ang’a alikana kukataa kulipa deni hilo, akisema:
“Mkinichokoza nitaondoka hapa niende Yerusalemu, hiyo mahali muichukue. Sijawahi kukataa kulipa hiyo ardhi, nawezaje kuendesha gari nzuri halafu nikatae kulipa? Sijakataa kulipa,” alisema kwa hasira.
Mhubiri huyo anayejulikana kwa kusema mambo bila kuficha alifafanua zaidi kuwa mgogoro huo uko mahakamani, jambo ambalo limekuwa chanzo cha mvutano kati yake na serikali ya kaunti.
“Kesi iko kortini, na nina barua kutoka kwa serikali. Sijui mna serikali ya aina gani. Serikali ilinipatia hiyo ardhi na ikaniandikia barua ikisema kwa sababu nafanya huduma ya ukombozi na kiwango ni kidogo, nisilipe. Sasa hamwezi kuandika barua nyingine ghafla na kusema huo msamaha umeisha leo, halafu iwe sawa.
Nyinyi ni watoto wadogo, hakuna mtu ninaogopa hapo. Mheshimu Mungu na mimi usinijaribu, mimi wachana na mimi,” alionya vikali.
Walichosema Wakenya mitandaoni:
chefmarkpro:
"Usiende Yerusalemu, nani atachapa wanaolala kanisani Mchungaji."
huyu_ni_wazim:
"Si alisema milioni kumi ni takataka."
mtwapa_finest_gallore:
"Commander akisema 'I swear before God' ujue mambo imekuwa mbaya."
whu_is_tutu:
"Nyinyi ni watoto 😂😂 mumezaliwa nikiwa hapo."
treasure bonareri:
"Ninapenda unabii 🙌 na iwe hivyo."
jusymtash:
"Heeee! Kumbe ni shamba ya commander mnataka kuchukua."
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke