Allois Cheruiyot Bett: Picha Zaibuka Kuonesha Jinsi Padri Aliyeuwawa Alivyohudumu kwa Utu

Allois Cheruiyot Bett: Picha Zaibuka Kuonesha Jinsi Padri Aliyeuwawa Alivyohudumu kwa Utu

  • Padri wa Kanisa Katoliki, Father Allois Cheruiyot Bett, alipigwa risasi na wanaume waliokuwa na silaha katika eneo la Tot, Bonde la Kerio, alipokuwa akielekea kuongoza ibada ya kanisani
  • Father Bett alifahamika sana kwa juhudi zake za kuleta amani na huduma zake zisizo na ubinafsi, mara nyingi akihubiri katika vijiji vya mbali katika mazingira ya unyenyekevu
  • Viongozi na wakazi walimwomboleza kama nguzo ya tumaini na imani, huku Mbunge Timothy Toroitich akielezea kifo chake kama dhabihu kwa ajili ya amani ya kudumu katika eneo hilo

Elgeyo Marakwet: Wanaume waliokuwa na silaha wanashukiwa kumuua kwa risasi Padri wa Kanisa Katoliki, Father Allois Cheruiyot Bett, katika eneo tete la Tot, Bonde la Kerio.

Allois Cheruiyot Bett: Picha Zaibuka Kuonesha Jinsi Padri Aliyeuwawa Alivyohudumu kwa Utu
Father Cheruiyot Bett akisherehekea misa kijijini. Picha: Timothy Toroitich.
Chanzo: Twitter

Kisa cha kusikitisha kilitokea Alhamisi, Mei 22, wakati padri huyo anaripotiwa kuwa njiani kwenda kuendesha ibada ya kanisa, kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet, Peter Mulinge.

Padri Bett, anayejulikana kwa juhudi zake zisizochoka za kuhimiza amani katika eneo lenye migogoro la Kerio Valley, anaombolezwa kama alama ya huduma ya kujitolea na imani thabiti.

Kifo chake kimesababisha mshtuko mkubwa katika jamii, ambako aliheshimiwa sana kwa kujitolea kwake katika huduma za kiroho, elimu, na upatanisho.

Mbunge wa Marakwet West aomboleza Padri Bett

Mbunge wa Marakwet West, Timothy Toroitich, alimtaja padri aliyeuawa kama rafiki wa karibu na mwanga wa matumaini.

“Padri Bett alikuwa mtu wa imani yenye uwezo wa kuhamisha milima. Alikuwa akinipigia simu mara kwa mara kushiriki maneno ya kutia moyo, hasa nyakati ngumu,” alisema Toroitich.

Kabla ya kuhamishiwa hivi karibuni katika Parokia mpya ya Tot, Padri Bett alihudumu katika Parokia ya Nerkwo.

Zaidi ya majukumu yake ya kichungaji, alikuwa mshauri muhimu katika maendeleo ya shule kuu za eneo hilo, zikiwemo Chebiemit Boys, Kapkoros Girls, Marakwet Boys, na Cheptulon Girls, akichangia katika maendeleo yao ya kitaaluma na ya maadili.

Je, Padri Cheruiyot Bett alikuwa mkarimu?

Padri Bett, aliyekuwa akiadhimisha mwaka wake wa pili katika ukuhani mwezi Novemba 2024, alisherehekea tukio hilo miezi michache iliyopita pamoja na familia moja ya kijijini Chepsirei, ambako walishiriki sala, keki, na furaha kama jamii moja.

Padri Bett akisherehekea na wasiojiweza katika hafla ya awali. Picha: Cheruiyot Bett.

Daima alikuwa mkarimu kwa jamii, akionyesha uongozi wa kuhudumia kwa maneno na vitendo.

Allois Cheruiyot Bett: Picha Zaibuka Kuonesha Jinsi Padri Aliyeuwawa Alivyohudumu kwa Utu
Father Allois Cheruiyot Bett akisherehekea na wasiojiweza wakati wa hafla iliyopita. Picha: Cheruiyot Bett.
Chanzo: Facebook

Hili lilionekana wakati wa maadhimisho hayo na katika kipindi chote cha utumishi wake katika eneo hilo.

Padri Bett ameombolezwa kama padri mwenye upendo.

Padri Cheruiyot Bett akitoa misaada kwa jamii katika hafla mbalimbali. Picha: Cheruiyot Bett.

Zaidi ya hayo, kujitolea kwake kulitambuliwa na utayari wake wa kuhubiri katika vijiji vya mbali, ambako mara nyingi aliendesha misa katika mazingira duni bila hata meza au mimbari.

Allois Cheruiyot Bett: Picha Zaibuka Kuonesha Jinsi Padri Aliyeuwawa Alivyohudumu kwa Utu
Padri Cheruiyot Bett aliwanunulia vyakula wasiojiweza. Picha: Cheruiyot Bett.
Chanzo: Facebook

Padri Bett aliingia vijijini kueneza ujumbe wa Mungu kwa upendo.

Akinukuu maneno maarufu ya Thomas Jefferson, Mbunge Toroitich alielezea matumaini kuwa kifo cha Padri Bett hakitakuwa bure.

“Damu iliyomwagika ya Padri Bett italinyunyizia mti wa amani katika Bonde la Kerio,” alisema, akiapa kuwa urithi wa padri huyo utaendelea kuishi kama kichocheo cha uponyaji na umoja katika eneo hilo.

Allois Cheruiyot Bett: Picha Zaibuka Kuonesha Jinsi Padri Aliyeuwawa Alivyohudumu kwa Utu
Padre Cheruiyot Bett akisherehekea misa kijijini. Picha: Cheruiyot Bett.
Chanzo: Twitter

Padri Cheruiyot Bett alikuwa na upendo wa kipekee kwa watoto.

Padri Allois Cheruiyot Bett wakati wa ibada (kushoto) na akiwa na jamii. Picha: Cheruiyot Bett.

Kwa sasa, huzuni imechukua nafasi ya furaha, huku wakazi wakitoa wito kwa serikali na vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka, thabiti, na makini kurejesha amani na kulinda maisha ya watu wasiokuwa na hatia katika eneo hilo.

Allois Cheruiyot Bett: Picha Zaibuka Kuonesha Jinsi Padri Aliyeuwawa Alivyohudumu kwa Utu
Allois Cheruiyot Bett wakati wa ibada iliyopita (kushoto) na wakati akishiriki na jamii. Picha: Cheruiyot Bett.
Chanzo: Facebook

Washukiwa 6 wa mauaji ya Padri Cheruiyot Bett wakamatwa

Wakati huohuo, washukiwa sita wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya padri huyo kwa kupigwa risasi.

Maafisa wa Kikosi Maalum cha GSU walijibu kwa haraka baada ya shambulio hilo na kuanzisha msako mara moja huku uchunguzi wa awali ukikanusha uhusiano wowote na wizi wa mifugo au ujambazi, na hivyo kuashiria kwamba nia ya mauaji inaweza kuwa tofauti.

Huduma ya Polisi ya Kitaifa imelaani mauaji hayo na kuahidi kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka ili kuwafikisha wote waliohusika mbele ya sheria.

Wakazi pia wamehimizwa kubaki watulivu, kuendelea na shughuli zao za kila siku, na kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama huku juhudi za kudumisha amani zikiongezeka katika eneo hilo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »