Allois Cheruiyot: Video ya Padri Aliyeuawa Akimuomba Ruto kwa Unyenyekevu Yaibuka

Allois Cheruiyot: Video ya Padri Aliyeuawa Akimuomba Ruto kwa Unyenyekevu Yaibuka

  • Padre Allois Cheruiyot, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana, alikuwa anajulikana kwa moyo wake wa kujitolea kwa waliomzunguka
  • Video moja inayomuonesha akitoa ombi la dhati kwa Rais William Ruto—si kwa ajili yake binafsi tu bali kwa niaba ya jamii nzima ya Elgeyo Marakwet—imesambaa sana mtandaoni
  • Hii inajiri siku moja baada ya rais kutoa heshima ya kihisia kwa marehemu padre huyo na kuahidi kuhakikisha haki inatendeka

Utulivu na mtazamo wa upole wa Padre Allois Cheruiyot Bett alipokuwa akizungumza na Rais William Ruto ulionyesha uwepo wa uhusiano wa karibu zaidi ya inavyoonekana.

Allois Cheruiyot: Video ya Padri Aliyeuawa Akimuomba Ruto kwa Unyenyekevu Yaibuka
Padre Allois Cheruiyot kwa ujasiri alitoa ombi kwa Rais William Ruto. Picha: William Ruto.
Chanzo: Facebook

Baada ya kifo chake, video isiyo na tarehe imejitokeza ikimuonesha marehemu padre akitoa ombi la dhati kwa kiongozi wa taifa, si kwa huduma yake tu, bali pia kwa mustakabali wa jamii yote ya Elgeyo Marakwet.

Padre Cheruiyot, ambaye alikuwa kasisi wa Parokia ya Mtakatifu Matthias Mulumba Tot, alipigwa risasi na wavamizi wasiojulikana siku ya Alhamisi, Mei 22, na kusababisha hofu na huzuni kubwa katika eneo hilo.

Je, Padre Allois Cheruiyot alimwomba nini Ruto?

Katika video hiyo, Cheruiyot alisema kuwa makasisi katika eneo hilo wana jukumu la “kufungua mioyo na akili,” kwa lengo la kubadilisha wale wenye nia mbaya.

Hata hivyo, alibainisha kuwa makasisi hukumbwa na changamoto kutokana na ukosefu wa usafiri katika eneo lenye vurugu za mara kwa mara na lisilo salama.

Cheruiyot alionekana kumwomba rais msaada wa magari ili kurahisisha harakati zao wanapotekeleza huduma yao.

"Wanaomba msaada ili waweze kusafiri kwa urahisi. Hata magari kwa ajili ya mikutano kama hii yangesaidia kuwaleta watu pamoja kuomba," alisema.

Aidha, marehemu padre alisema kuwa makanisa ya eneo hilo huwasaidia wasiojiweza lakini yanahitaji msaada wa serikali ili kuendelea na kazi hiyo.

“Makanisa haya hapa chini, licha ya kuhubiri amani, pia huwasaidia wale wasiojiweza. Tuna makanisa kama AIC kule Arror yanayosaidia yatima kupata elimu. Kanisa la Baptist kule Tot nalo linatoa msaada huo huo. Wanatoa mchango mkubwa kwa walio na uhitaji,” alisema Cheruiyot.

“Tunashukuru serikali kwa kujali wasiojiweza. Tukisaidia huduma ya hawa makasisi ya kufungua mioyo na akili, na pia kuwaunga mkono wasiojiweza, itakuwa msaada mkubwa kwa ufalme wa Mungu,” aliongeza.

Subscribe to watch new videos

Je, William Ruto alimwomboleza Cheruiyot?

Kifo cha Cheruiyot kilileta huzuni kubwa nchini, kikiwa kimetokea siku chache tu baada ya kuuawa kwa kikatili kwa Padre John Maina wa Parokia ya Katoliki ya Igwamiti huko Nyandarua.

Rais alijiunga na Wakenya kumuomboleza Cheruiyot na akaahidi kuwa mamlaka zitawasaka waliotekeleza mauaji hayo na kuhakikisha wanakabiliwa na haki.

“Mungu awape familia na marafiki nguvu ya kustahimili kifo hiki chenye uchungu. Tutawatafuta wauaji wake huku tukiendelea kuahidi kurejesha amani katika Bonde la Kerio,” alisema Ruto.

Mapadre na masista waomboleza kifo cha Padre Cheruiyot

Katika tukio tofauti, video iliyowaonesha mapadre na masista wakiomboleza kifo cha Cheruiyot ilisambaa sana na kugusa nyoyo za Wakenya kote nchini.

Allois Cheruiyot: Video ya Padri Aliyeuawa Akimuomba Ruto kwa Unyenyekevu Yaibuka
Padre Allois Cheruiyot alipendwa sana na wenzake kazini, waliomwomboleza kwa huzuni kubwa. Picha: Rev. Petros Mwale.
Chanzo: Facebook

Video hiyo ilionyesha huzuni ya kina ya makasisi wenzake walipokuwa wakilia kutokana na kifo cha ghafla cha padre huyo.

Walikusanyika pamoja na wakazi wa kijiji cha Tot katika Bonde la Kerio, eneo la Mokoro, Kata Ndogo ya Kakiptul, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, kumuenzi marehemu padre huyo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Francis Silva avatar

Francis Silva (Swahili translator) Francis M Silva ni Mkuu wa Kitengo cha Kiswahili. Ana tajriba ya miaka mingi katika taaluma ya uwanahabari hasa tafsiri, uhariri - Radio, TV na Dijitali. Yeye ni zao la Taasisi ya Mawasiliano-Umma ya Kenya (KIMC). Wasiliana naye kupitia: [email protected]

OSZAR »