Polisi Wakanusha Kuhusika Katika Kumteka Nyara Mbunge wa Juja George Koimburi: “Ni Vitimbi Tu”
- Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) inakanusha madai ya kutekwa nyara na kuteswa kwa Mbunge wa Juja George Koimburi kwenye video inayosambazwa mitandaoni
- Msemaji wa polisi Muchiri Nyaga anasema Koimburi alijificha kimakusudi ili kukwepa kukamatwa kwa sababu ya kesi ya ulaghai wa ardhi inayomkabili
- Mbunge huyo wa Juja anadaiwa kutoroka wavu wa polisi akiwa kwenye pikipiki na kuibuka tena Jumatatu, Mei 26, baada ya kutoweka kwa siku kadhaa
Nairobi - Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) imetoa taarifa kuhusiana na video inayosambazwa mitandaoni ya madai ya kutekwa nyara kwa Mbunge wa Juja George Koimburi.

Chanzo: Facebook
Je, polisi walimteka nyara mbunge George Koimburi?
Katika taarifa ya Jumatatu, Mei 26, msemaji wa polisi Muchiri Nyaga alipuuzilia mbali madai kwamba maafisa wa usalama walimteka nyara na kumtesa mbunge huyo kabla ya kumtupa katika shamba la kahawa huko Kiambu.
Ngaga alisema kuwa mbunge huyo wa Juja alikwepa kukamatwa kwa makusudi kuhusiana na uchunguzi unaoendelea wa ulaghai wa ardhi.
Idara ya polisi ilisema kwamba Koimburi alijificha baada ya kufahamu kuwa maafisa walipanga kumkamata Ijumaa, Mei 23, kufuatia idhini kutoka kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) kumfungulia mashtaka.
"Mbunge huyo, baada ya kujua nia ya polisi kumkamata, alikwepa wavu na kuwahadaa maafisa kwa kutoroka kwa pikipiki na usalama wake wa kibinafsi na kuzima simu yake ya rununu," Nyaga alisema.
Kulingana na NPS, mbunge huyo wa Juja, ambaye hakupatikana wikendi, aliibuka tena Jumatatu huku kukiwa na madai ya kutekwa nyara.
Sasa, ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) inachunguza video hiyo ya uwongo ili kubaini ukweli wa madai ya kutekwa nyara.

Chanzo: Facebook
Polisi wanasema maafisa kutoka Juja walitembelea eneo lililoonyeshwa kwenye video, na eneo hilo 'limerekodiwa ipasavyo' ili kusaidia katika uchunguzi.
"Mbunge huyo aliibuka tena leo huku kukiwa na madai ya kutekwa nyara. Polisi kutoka Juja walitembelea eneo linalodaiwa kuwa eneo la tukio na kuweka kumbukumbu. Kikosi maalum kutoka makao makuu ya DCI kinachunguza video hiyo ya uwongo na hali zote zinazohusiana na madai ya kutekwa nyara," Nyaga alisema.
NPS inamtaka mtu yeyote aliye na habari kuhusu video ya Koimburi kupatikana katika shamba la kahawa kujitokeza na kusaidia polisi katika uchunguzi unaoendelea.
"Huduma ya Kitaifa ya Polisi inamtaka yeyote aliye na habari kuhusu tukio lililoonyeshwa kwenye video kujitokeza na kusaidia katika uchunguzi," msemaji wa polisi alisema.
Je, mbunge George Koimburi aliteswa?
Katika habari zinazohusiana na hizo, aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua na viongozi kadhaa kutoka Chama cha Demokrasia kwa Wananchi (DCP) walimtembelea Koimburi katika Hospitali ya Karen.
Akizungumza na wanahabari, Gachagua alisema madaktari wamethibitisha kuwa mbunge huyo wa Juja alipata majeraha ya tishu laini yaliyosababishwa na mateso ya kikazi.
Naibu rais huyo wa zamani pia alidai kuwa Koimburi alidungwa kemikali hatari ambayo imeathiri uwezo wake wa kuzungumza.
Gachagua alieleza kuwa Koimburi aliwasilisha maelezo hayo kwa maandishi, kwani kwa sasa hawezi kuzungumza.
Kiongozi huyo wa DCP aliongeza kuwa sampuli za damu na mkojo kutoka Koimburi zimetumwa kwa maabara za kibinafsi kwa uchunguzi zaidi ili kubaini dutu inayohusika.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke