Video: Babake Albert Ojwang Azungumza Kwa Huzuni Baada ya Ripoti ya Uchunguzi wa Maiti Kutolewa
- Daktari wa upasuaji Bernard Midia alithibitisha kuwa Albert Ojwang alifariki kutokana na majeraha ya kichwa, kubanwa shingoni, na majeraha mbalimbali yanayoendana na kushambuliwa, akipinga madai ya awali ya polisi
- Meshack Opiyo alimtaka Eliud Lagat kutoa majibu, akihoji ni kwa nini mwanawe alilengwa na kuuawa kwa madai ya ufisadi ilhali wengine waliotajwa bado wako huru
- Aliitaka serikali ya Rais William Ruto itende haki na akalaani ripoti ya uongo ya polisi ambayo anaamini ilitumika kuficha mauaji hayo
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Nairobi: Albert Ojwang, aliyefariki akiwa korokoroni katika Kituo cha Polisi che Central, alishambuliwa kimwili na alipata majeraha mbalimbali mwilini mwake, kulingana na matokeo ya daktari wa upasuaji wa serikali.

Chanzo: TikTok
Baada ya uchunguzi wa maiti uliofanywa Jumanne, Juni 9, Daktari wa serikali wa upasuaji, Bernard Midia, alihitimisha kuwa kifo cha Albert Ojwang’ kilisababishwa na majeraha ya kichwa, kubanwa shingoni, na majeraha yaliyosambaa mwilini viashiria wazi vya kupigwa.
Matokeo ya upasuaji yanapingana moja kwa moja na madai ya awali ya polisi kwamba Ojwang’ alijijeruhi kwa kujigonga ukutani.
Midia alisema kuwa muundo wa majeraha hauendani na tukio kama hilo.
Babake Albert Ojwang’ aumia baada ya ripoti ya upasuaji
Babake marehemu, Meshack Opiyo, alizungumza kwa uchungu mkubwa baada ya kutolewa kwa ripoti ya upasuaji.
Akijitahidi kuzuia machozi, Opiyo alielekeza hasira na huzuni yake kwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Eliud Lagat, ambaye alimtuhumu kupanga kukamatwa kwa mwanawe na maafisa wa DCI.
“Nilikabidhi mwana wangu kwa heshima, nikiwa na imani na sheria na uongozi,” alisema. “Sasa ripoti ya upasuaji inaonyesha alikufa kwa majeraha aliyopewa na watu wale wale waliomchukua. Nataka majibu kwa nini mwana wangu aliuliwa? Alikosa nini kiasi cha kustahili kifo?”

Chanzo: Facebook
Opiyo alishangaa ni kwa nini mwanawe, ambaye alikuwa akizungumza kuhusu ufisadi suala linaloathiri taifa zima ndiye aliyepatwa na mauti ya kikatili, ilhali wengi waliotajwa katika ufisadi bado wako huru.
“Nilitumia nguvu zangu zote kumsomesha mwanangu huko Kilifi, nikitoka jasho kwenye machimbo, nikijinyima sana. Alipohitimu, niliona mwanga wa msaada kwangu,” alisema. “Sasa nimebaki na sifuri mkono wangu umevunjika, moyo wangu umesagika. Nimenusurika kimwili lakini nimekufa ndani. Kwa nini mliniondolea mwana wangu?”
Alikanusha vikali madai ya polisi ya awali kwamba Ojwang’ alijijeruhi mwenyewe kwa kujigonga ukutani, akieleza kuwa haiwezekani majeraha yaliyopatikana chini ya mikono yake yamejifanyiwa mwenyewe.
“Hili halikuwa ajali,” alisema.
“Rais William Ruto, nisaidie. Mimi ni maskini, lakini mlipa ushuru. Siwezi kupigana na hii vita peke yangu. Walipiga picha za nyumba yangu na hapo ndipo walinilenga. Kile kilichonipata ni laana.”
Opiyo anatoa wito wa haki na uwajibikaji katika kifo hiki kilichosababisha hasira kubwa kwa umma na kuibua upya hofu kuhusu ukatili wa polisi na namna mahabusu wanavyotendewa nchini Kenya.
Nini kilimfanyikia mamake Albert Ojwang’?
Wakati huohuo, mama wa Ojwang’ alizirai baada ya kupokea taarifa za kifo cha mwanawe akiwa katika mazishi ya shemeji yake.
Kulingana na baba yake Ojwang’, mama huyo sasa yuko katika hali dhaifu na kimya, akiwa hawezi hata kuzungumza kutokana na mshtuko wa huzuni uliompata.
Familia na majirani wanaendelea kumpa msaada na faraja huku nyumba hiyo ikikumbwa na huzuni kubwa ya misiba miwili kwa mpigo.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke