Albert Ojwang: Korti Yamzuilia OCS Samson Talaam kwa Siku 15 Kuhusiana na Kifo cha Bloga

Albert Ojwang: Korti Yamzuilia OCS Samson Talaam kwa Siku 15 Kuhusiana na Kifo cha Bloga

  • Hakimu wa Mahakama ya Milimani Ben Mark Ekhubi alikubali ombi lililowasilishwa na Mamlaka Kuchunguza Utendakazi wa Polisi (IPOA)
  • IPOA ilidai kuwa OCS wa Kituo cha Polisi cha Central, Samson Talaam, anaweza kuwavuruga mashahidi walioachiliwa kwa dhamana
  • Talaam anatuhumiwa kushiriki katika kupanga mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang

Nairobi - Mahakama imewaruhusu polisi kuendelea kumzuilia OCS wa Kituo cha Polisi cha Central, Nairobi Samson Talaam kwa siku 15 zaidi.

Samson Talaam
Albert Ojwang: Korti Yamzuilia OCS Samson Talaam kwa Siku 15 Kuhusiana na Kifo cha Bloga.
Chanzo: Original

Kwanini Samson Talaam alinyimwa dhamana?

Mnamo Jumatano, Juni 18, Hakimu wa Mahakama ya Milimani Ben Mark Ekhubi aliamuru Talaam azuiliwe kwa siku 15 ili kuruhusu uchunguzi wa mauaji ya mwanablogu Albert Omondi Ojwang.

Ekhubi aliagiza OCS huyo azuiliwe katika Kituo cha Polisi cha Lang’ata ili kuruhusu Mamlaka Kuchunguza Utendakazi wa Polisi (IPOA) kukamilisha uchunguzi wao.

Katika uamuzi wake, hakimu huyo alidai kuwa upande wa mashtaka ulitoa sababu za kutosha kuhalalisha kuzuiliwa kwa Talaam kwa muda mrefu.

IPOA ilidai kuwa mshukiwa ana ushawishi na mamlaka, na kumwachilia kunaweza kuingilia uchunguzi na mashahidi.

Aliongeza kuwa cheo cha juu cha Talaam na utumishi wa muda mrefu katika kikosi hicho kilimpa fursa ya kupata uwezo wa kumzuia dhidi ya uwajibikaji na kuathiri uchunguzi.

"Msimbo wa bluu ni jambo la kawaida katika safu za polisi - hata katika mamlaka kama Marekani. Mtuhumiwa anaongoza kituo kikubwa zaidi cha polisi nchini na ana mtandao mkubwa. Kuna hatari ya kuaminika kwamba anaweza kuingiliana na mashahidi au ushahidi," Ekhubi aliamua.

Wakili wa Talaam alidai kuwa siku 15 zinapaswa kuhesabiwa kuanzia Juni 13, tarehe ambayo alitiwa mbaroni kwa mara ya kwanza lakini mahakama iliagiza muda huo uanze kuhesabiwa Juni 16.

Unachohitaji kujua kuhusu kesi ya mauaji ya Albert Ojwang

  • Mkuu wa DCI Amin Mohamed aliwaambia maseneta kuwa Samson Taalam, afisa mkuu wa Kituo cha Polisi cha Central, anatakiwa kuchukuliwa kama mshukiwa mkuu wa mauaji ya Ojwang.
  • Konstebo wa polisi James Mukhwana alikiri kupanga mateso ya Albert Ojwang kutokana na maagizo yanayodaiwa kutolewa na OCS Talaam na DIG Eliud Lagat.
  • Uchunguzi wa maiti uliofanywa na wanapatholojia wa serikali ulifichua kwamba alikuwa amepata kiwewe cha nguvu, majeraha ya ndani ya kichwa na dalili za kunyongwa shingoni

taalam
OCS Samson Talaam atazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Lang'ata. Picha: NPS.
Chanzo: Facebook

Je, Samson Talam anahusishwa vipi na mauaji ya Albert Ojwang?

Kama ilivyoripotiwa awali, IPOA, kupitia kwa afisa Abidirahman Jibril, iliwasilisha nyaraka zinazosimulia jinsi Talaam anahusishwa na mauaji ya kikatili ya Ojwang.

Katika hati yake ya kiapo, Jibril alidai kuwa OCS wa Kituo Kikuu cha Polisi anahusishwa na mauaji ya kinyama ya Ojwang.

Kulingana na stakabadhi zilizowasilishwa na IPOA, Talaam alidaiwa kuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara na Polisi Konstebo Juma Mukhwana, mshukiwa mwingine wa kesi hiyo, usiku ambapo mwanablogu huyo aliuawa.

Katika nyaraka hizo za mahakama, IPOA ilidai kuwa siku hiyo, Talaam alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na watu waliokuwa nje ya kituo hicho, akidaiwa kuwapa taarifa kuhusu matokeo ya mauaji hayo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »