Polisi Watoa Taarifa Kuhusu Video Iliyowanasa Maafisa Wakitoweka na Vipatakilishi Vilivyoibwa
- Maafisa wa polisi wa kupambana na fujo walinaswa kwenye video wakiondoka na tarakilishi mpakato zilizoibwa kutoka kwa duka la vifaa vya elektroniki na magaidi wakati wa maandamano ya Jumanne, Juni 17
- Video hiyo ilizua hisia tofauti, huku baadhi wakihoji kitendo cha maafisa hao wa polisi huku wengine wakisema kuwa kompyuta hizo zilichukuliwa kutoka kwa majambazi
- Kufuatia haya, Huduma ya Kitaifa ya Polisi imeweka sawa jinsi matukio yalivyotokea, na kusababisha polisi kuonekana na vipatakilishi hivyo
Huduma ya Kitaifa ya Polisi hatimaye imevunja ukimya wake kuhusu kanda ya video iliyonasa maafisa waliovalia sare wakiendesha gari wakiwa na tarakilishi mpakato.

Chanzo: Getty Images
Je, polisi walipeleka tarakilishi mpakato zilizoibiwa kwenye Kituo cha Polisi cha Central?
Katika taarifa siku ya Jumatano, Juni 18, Idara ya polisi ilifafanua kuwa kufuatia maandamano ya Jumanne, maduka kadhaa yalivunjwa na vitu vya thamani kuibwa.
Aidha NPS ilisema katika kipindi hicho, waliweza kumkamata mshukiwa mmoja na kupata laptop nne, ambazo kwa sasa ziko chini ya ulinzi wa polisi kama vielelezo katika Kituo Kikuu cha Polisi.
"Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) imebaini video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikionyesha afisa wa polisi akiwa ameshikilia kompyuta mpakato. NPS inapenda kufafanua kuwa kufuatia maandamano ya hivi majuzi jijini Nairobi, maduka kadhaa yalivunjwa na vitu mbalimbali kuibiwa," taarifa hiyo ya polisi ilisoma kwa sehemu.
Polisi waliwataka Wakenya ambao maduka yao yalivunjwa na kuibiwa kompyuta mpakato kuripoti kituoni, ambapo wataweza kubaini vitu vilivyopatikana.
"Wakati huo huo, uchunguzi unaendelea ili kubaini na kuwakamata wale waliohusika katika shughuli za uhalifu wakati wa maandamano," NPS ilisema zaidi.
NPS pia ilisisitiza kujitolea kwake kutekeleza jukumu lake la kulinda Wakenya na mali zao. Kabla ya ufafanuzi wa NPS, picha za video zilizua ghadhabu huku baadhi ya Wakenya wakihoji nia ya maafisa hao.
Hata hivyo, Wakenya wengine walieleza haraka kuwa maafisa hao walikuwa wamezipata kompyuta hizo kutoka kwa wahuni ambao walikuwa wameharibu duka la vifaa vya elektroniki huko Nairobi CBD.
Chanzo: TUKO.co.ke