Video: Mwandamanji Alipuliwa Mikono na Kitoa Machozi Wakati wa Maandamano ya Gen Z

Video: Mwandamanji Alipuliwa Mikono na Kitoa Machozi Wakati wa Maandamano ya Gen Z

  • Wakenya walimiminika mitaani kuandamana kwa ajili ya kuwaenzi vijana wa Gen Z waliopoteza maisha yao wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa mwaka 2024
  • Katika harakati za kuwatawanya vijana waliokuwa wakiandamana katikati ya jiji la Nairobi, maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia walirusha mabomu ya machozi
  • Kijana mmoja alichukua mojawapo ya mabomu hayo kwa lengo la kulirudishia polisi, lakini kwa bahati mbaya, lililipuka mikononi mwake

Nairobi: Tukio la kuhuzunisha limetokea katikati mwa jiji la Nairobi baada ya bomu la machozi kulipuka mikononi mwa mwandamanaji wakati wa maandamano ya Gen Z.

Video: Mwandamanji Alipuliwa Mikono na Kitoa Machozi Wakati wa Maandamano ya Gen Z

Kitoa machozi hicho kililipuka baada ya waandamanaji kukichukua kufuatia afisa wa polisi wa kupambana na ghasia kulifyatua ili kuwatawanya waandamanaji.

Kijana huyo alikusudia kulirejesha bomu hilo kwa maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia, lakini kwa bahati mbaya, mikono yake ililipuliwa.

Video ilionyesha waandamanaji wengine wakimsaidia kwa kumfungia mikono kwa kitambaa kabla ya kumpandisha pikipiki na kumkimbiza kituo cha afya.

"Tafadhali, tafadhali... Usijali, utapona. Tafadhali tumchukue twende hospitali," alisikika akisema mhudumu wa kwanza kufika kumsaidia.

Mwanaume mwingine alionekana akiwaonya waandamanaji dhidi ya kushika mabomu ya machozi mara tu yanapofyatuliwa na polisi.

"Msishike teargas tena! Pole sana, mahn, pole," mtu mmoja alisikika akisema.

Wanaume wawili wapigwa risasi wakati wa maandamano

Wakati huo huo, wanaume wawili wamekimbizwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia.

Video zilizosambaa mitandaoni zilionyesha mmoja wa wanaume hao akiwa analia kwa maumivu baada ya kujeruhiwa kwa risasi, wakati alipokuwa akipokelewa na wahudumu wa afya katika KNH.

Mmoja wa waandamanaji aliyehusika katika kuwasaidia kuwasafirisha majeruhi hospitalini alisimulia jinsi tukio hilo lilivyotokea.

Alidai kuwa kundi la maafisa watano wa polisi liliwazingira na kuanza kuwashambulia.

Mwandamanaji huyo alieleza kuwa mmoja wa wanaume hao alijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi kichwani.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »