Mbunge wa ODM Awasihi Wenyeji Wamruhusu Amuunge Mkono William Ruto: "Msinipige Mawe"

Mbunge wa ODM Awasihi Wenyeji Wamruhusu Amuunge Mkono William Ruto: "Msinipige Mawe"

  • Mbunge wa Lugari, Nabii Nabwera, aliwaomba wapiga kura wake wamruhusu afanye kazi na Rais William Ruto, akitaja ahadi za maendeleo zilizotolewa kwa eneo hilo
  • Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Nabwera alisema kuwa Ruto aliahidi kujenga barabara kuu za lami katika Lugari, na iwapo ahadi hiyo itatekelezwa, hatakuwa na budi ila kumuunga mkono rais huyo
  • Mbunge huyo wa ODM alitumia methali ya kitamaduni kuelezea msimamo wake wa kisiasa, akifananisha mkataba wa Ruto na Raila na kumkubali mama mpya katika familia

Katika ombi la ujasiri lililopambwa na hekima, Mbunge wa Lugari, Nabii Nabwera, alitoa hoja isiyo ya kawaida kwa wapiga kura wake.

Mbunge wa ODM Awasihi Wenyeji Kumruhusu Amuunge Mkono William Ruto: "Msinipige Mawe"
Mbunge wa Lugari Nabii Nabwera aliwaomba wapiga kura wake kumruhusu kumuunga mkono Rais William Ruto. Picha: Nabii Nabwera.
Chanzo: Facebook

Aliwahimiza wakaaji kumuunga mkono katika nia yake ya kushirikiana na Rais William Ruto, ikiwa hilo litaleta maendeleo yaliyosubiriwa kwa muda mrefu katika eneo hilo.

Mbunge huyo wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) alikuwa akizungumza na wakazi wakati wa mkutano wa hadhara eneo la Lugari, kaunti ya Kakamega, ambapo aliwataka wakaaji waunge mkono uamuzi wake, akisisitiza kuwa siasa inapaswa kuhudumia maslahi ya maendeleo.

Mbunge huyo alifichua kuwa Ruto aliahidi kutandika lami barabara muhimu katika eneo hilo, na akaeleza kuwa uungwaji mkono wake kwa rais utategemea utekelezaji wa ahadi hizo.

“Ruto ni jirani yangu. Akitimiza ahadi ya ujenzi wa barabara za Turbo na Luandeti, sitakuwa na budi ila kuwa mfuasi wake,” Nabwera alisema.

Aliwaomba wakaaji wasimgeukie, akisisitiza kuwa uaminifu wa kisiasa bila manufaa halisi hauna maana.

“Siasa bila maendeleo ni upumbavu. Huwezi kula maneno matupu,” alisema kwa msisitizo.

Mbunge wa Lugari hana furaha na wakaaji wanaomuunga mkono Gachagua

Nabwera alieleza kufadhaishwa na baadhi ya wakaaji wanaoendelea kumuunga mkono naibu rais wa zamani Rigathi Gachagua, ambaye alimshutumu kwa kuzuia juhudi za kukamilisha miradi ya barabara.

Alidai kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo, ambazo zilipaswa kukamilika mwaka 2023, zilielekezwa kwingine wakati Gachagua akiwa madarakani.

Akigusia msimamo wake wa kisiasa kwa upana zaidi, Nabwera alitoa mfano wa kitamaduni kuelezea mabadiliko ya hali ya kisiasa nchini.

Aliifananisha ushirikiano kati ya kiongozi wa ODM Raila Odinga na Ruto na baba anayeleta mke mpya nyumbani.

“Kwa tamaduni zetu, unaweza kukataa kumkubali mama yako akiwa bado nje, lakini baba akimleta ndani, huyo ndiye mama yako sasa. Raila ni baba yangu wa kisiasa, na sasa ameolewa na Ruto, kwa hivyo ni vigumu kwangu kusema siwezi kuwa upande wa Ruto,” alieleza.

Kauli za Nabwera zinaonyesha mwelekeo mpya wa baadhi ya wanasiasa wa ODM kuanza kuikaribia serikali ya Kenya Kwanza.

Nabii Nabwera anataka kumuunga mkono Ruto

Mbunge wa ODM, Nabii Nabwera, aliunga mkono ushirikiano kati ya chama chake na serikali ya Kenya Kwanza. Picha: Nabii Nabwera.

Mbunge wa ODM Awasihi Wenyeji Kumruhusu Amuunge Mkono William Ruto: "Msinipige Mawe"
Mbunge wa ODM Nabii Nabwera alikaribisha mapatano ya kazi ya chama na serikali ya Kenya Kwanza. Picha: Nabii Nabwera.
Chanzo: Facebook

Je, Raila yuko katika serikali ya Ruto?

Katika taarifa nyingine iliyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Raila alisisitiza kuwa yeye si sehemu ya serikali, licha ya wanachama wa ODM kushikilia nyadhifa kuu serikalini.

Akizungumza wakati wa mkutano wa 42 wa ICPAK mjini Mombasa, kiongozi huyo wa ODM alifafanua kuwa chama chake kilitoa tu wataalamu kusaidia serikali ya Kenya Kwanza kusimamia uchumi.

Alisisitiza kuwa ushiriki wa ODM usitafsiriwe kama kujiunga rasmi na serikali.

Alitaja kuwa viongozi kama John Mbadi, Hassan Joho, Wycliffe Oparanya, na Opiyo Wandayi walipelekwa katika Baraza la Mawaziri la Ruto kwa lengo la kuleta utulivu nchini, si kama ishara ya uungwaji mkono wa kisiasa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »