Morara Kebaso Ajitoa Katika Ulingo wa Siasa, Adai Nusra Awe Kichaa: "Hakuna Anayeweza Kunihukumu"

Morara Kebaso Ajitoa Katika Ulingo wa Siasa, Adai Nusra Awe Kichaa: "Hakuna Anayeweza Kunihukumu"

  • Morara alitangaza meachana na siasa, akisherehekea uhuru anaoupata wa kuishi bila kuhukumiwa
  • Morara alisema sasa anaweza kuangazia biashara yake, kufurahia maisha, kusafiri, na kuishi bila shinikizo la umma
  • Alisherehekea na kueleza kuwa hatakuwa tena chini ya uangalizi wa mara kwa mara, ikiwemo kutohitaji ulinzi au kukabiliwa na mahojiano ya runinga

Kiongozi wa chama cha Inject Party of Kenya, Morara Kebaso, ameachana na siasa.

Morara Kebaso Ajitoa Katika Ulingo wa Siasa, Adai Nusra Awe Kichaa: "Hakuna Anayeweza Kunihukumu"
Morara Kebaso asherehekea baada ya kuacha siasa. Picha: Morara Kebaso.
Chanzo: Twitter

Katika ujumbe wake mitandaoni Morara alisema sasa anaweza kuishi maisha yake, kufanya biashara zake na kutengeneza pesa zake kwa amani bila kuchunguzwa na umma.

Alisema sasa yuko huru na hakuna mtu anayeweza kumhukumu kwa njia yake ya kuishi.

"Wasee 😀 hatimaye nimekwepa siasa. Sasa naweza kuishi maisha yangu. Nafanya biashara zangu, natafuta mulla, nasafiri duniani, naona marafiki zangu, naenda bar bila kuwa na wasiwasi wa kupigwa picha. Niko huru. Hakuna anayenihukumu nikicheza vibaya au nikitabasamu vibaya," Morara alisema.

Mfanyabiashara huyo aliongeza kuwa hatahitaji walinzi, ataendesha gari lake mwenyewe, na hatapokea mialiko ya mahojiano ya runinga.

"Sihitaji ulinzi. Naweza kuendesha gari langu na kukimbia kama upepo. Sitahitaji kufika kwenye mahojiano ya runinga na kunukuliwa vibaya. Sitajali kuhusu mitandao ya kijamii au maneno ya watu ambao hawajafikia hata nusu ya mafanikio yangu nikiwa na umri mdogo. 😄 Wooooh. Inafurahisha. Fantabulous kabisa. Sihitaji kuelezea mtu gharama ya shati langu, viatu, gari au nyumba yangu kwa sababu siyo biashara yao," Morara aliongeza.

Je, Morara Kebaso alilemewa na siasa?

Ni wazi kuwa Morara alilemewa na mzigo wa siasa na shinikizo lililokuwa nalo.

Alisherehekea kuwa sasa ataabudu kwa uhuru na kuhubiri neno la Mungu bila watu kumwona kama anatafuta kiki.

Morara alifichua kuwa karibu apate kichaa kwa sababu ya siasa.

"Sasa naweza kuabudu kwa uhuru na kuhubiri neno la Mungu bila mtu kudhani ninasaka umaarufu au kuigiza. Huu ni mwepuko wa kweli. Nilikuwa karibu kupagawa. Naweza kuishi maisha yangu sasa wasee, 😀😀😀hatimaye. Naweza sikia Amen huko nyuma?" Morara alihitimisha.

Morara Kebaso Ajitoa Katika Ulingo wa Siasa, Adai Nusra Awe Kichaa: "Hakuna Anayeweza Kunihukumu"
Morara Kebaso alisek kanisa hata mambo na siasa tena. Picha: Morara Kebaso.
Chanzo: Twitter

Maoni ya mashabiki wake yalikuwa tofauti:

Bett Kuchez:

"Poapoa Morara. Kwa nini ubebe dhambi za watu wasio na shukrani? Sisi tulia."

Simon Siro:

"Hatua nzuri.. nahisi ulipewa ushauri bora. Umefunga milango yote ya siasa. Pumzika kisha urudi kwa nguvu."

Around the Rift Valley:

"Rudisha milioni zetu za michango kabla hujatusema vibaya namna hii."

John Kimathi:

"Angalau tumeondolewa mzigo wa harambee zisizoisha."

Psychotomimetic Vincent:

"Hakuna aliyekuwa na hamu na wewe katika siasa."

Kevin Sultan Ombongi:

"Misheni imekamilika..mcheza vizuri hujua wakati wa kutoka jukwaani. Vinginevyo, ulionekana msaliti mwenye mradi..kula vizuri ulichochuma."

Morara Kebaso azungumza kuhusu makosa aliyowahi kufanya?

Hapo awali, Morara alifunguka kuhusu safari yake ya kibiashara, akieleza makosa aliyowahi kufanya.

Mwanasiasa huyo, ambaye anadai kuwa na utajiri wa KSh milioni 100, alisimulia jinsi alivyowahi kuchukua mkopo wa gari kutoka kwa taasisi ya kifedha ya microfinance.

Alikiri pia kuwa alikosea kwa kuichukulia M-Pesa kama taasisi ya kifedha, jambo lililomzuia kupata mkopo kutoka kwa benki alipowasilisha stakabadhi za miamala ya M-Pesa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »