Video ya Bintiye Salva Kiir Akizungumza Kuhusu Maisha Yake Nchini Kenya Yaibuka:"Sikujua Kiingereza"

Video ya Bintiye Salva Kiir Akizungumza Kuhusu Maisha Yake Nchini Kenya Yaibuka:"Sikujua Kiingereza"

  • Adut Salva Kiir Mayardit alisema alizuru Kenya kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 10 na hakuwa na ujuzi wa kuzungumza Kiingereza
  • Hakuna aliyemlazimisha kwenda shule, lakini kiu chake cha maarifa na taarifa ndiyo kilichomfanya kuamka kila siku na kusoma
  • Binti huyo wa Rais wa Sudan Kusini aliwaonya wasichana wa shule kuepukana na mahusiano mpaka watakapokamilisha elimu yao

Video ya Adut Salva Kiir Mayardit, bintiye Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit, akifunguka kuhusu maisha yake nchini Kenya imeibuka.

Video ya Bintiye Salva Kiir Akizungumza Kuhusu Maisha Yake Nchini Kenya Yaibuka:"Sikujua Kiingereza"
Adut Salva Kiir (kulia) na babake Rais Salva Kiir (r). Picha: Odhiambo Levin Opiyo, Wizara ya Masuala ya Kigeni, Sudan Kusini (Facebook).
Chanzo: Facebook

Wakati wa ziara yake nchini Afrika Mashariki, Adut alikuwa akitia matumaini na hekima katika maisha ya vijana.

Alizungumza na wasichana wa shule kuhusu umuhimu wa elimu, akishiriki uzoefu wake binafsi alipokuwa akiishi katika nchi ya kigeni.

Adut alitembelea Kenya lini?

Adut alikuja Kenya hasa kuendeleza elimu yake baada ya kuhudhuria shule mbalimbali nchini Ethiopia.

"Nilisoma katika shule za Ita, Gambela, na Addis Ababa. Tulipofika Kenya, nakumbuka nilikuwa na umri wa miaka 10. Sikuwa najua Kiingereza. Sijui kwa nini sikuweza kuzungmza Kiingereza, lakini nilizungumza Nuer, Shilluk, Dinka, na Kiamhari. Nilikuwa na marafiki kutoka kila kona ya maisha ndani ya kambi huko Ita. Ningeweza kuzungumza lugha hizo zote, isipokuwa Kiingereza.

Nilijiunga na darasa lenye wanafunzi 55, na nakumbuka nilikuwa wa 53 kati ya 55 katika muhula wangu wa kwanza. Bila shaka, mjomba wangu aliniambia, 'Lazima ufanye bidii na usome kwa bidii,’ lakini kwa upande wangu, ilikuwa ni nchi mpya. Sikuwa najua Kiswahili pia," alisema.

Hamu ya Adut ya kusoma

Katika muhula wa pili, Adut alionyesha maendeleo makubwa katika masomo yake, akapanda hadi nafasi ya 20 kati ya 55.

Aliongeza kuwa hakuna mtu aliyemlazimisha kwenda shule, bali hamu ya kujifunza na kupata maarifa ndiyo iliyomsukuma kufanya juhudi.

"Nilikuwa na hamu ya kwenda shule. Ningeamka, nivae sare yangu, na niende shule. Nilikuwa kimya—sikuwa mtoto wa kuongea sana—lakini nakumbuka nilitamani sana kujifunza. Hamu hiyo haikupandikizwa kwangu kwa nguvu au adhabu," alisema.

Adut awaonya wasichana wa shule kuhusu mahusiano ya kimapenzi

Adut alidai kwamba yeye na ndugu zake hawakumsumbua mama yao, kwani walitaka aendelee kuwa na afya njema kwa miaka mingi.

Alieleza kuwa hakuhitaji kuadhibiwa ili aelewe kwamba hafai kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi akiwa bado shuleni.

"Kwa wale mnaopenda kuwa katika wapenzi, sijui mnayaweza vipi, lakini singewashauri hivyo. Mkae mbali na mahusiano hadi mtakapokomaa," alishauri.

Je, rais wa Sudan Kusini amefariki?

Katika taarifa tofauti, serikali ya Sudan Kusini ilikanusha uvumi kuwa rais wao amefariki, ikiwahakikishia wananchi kuwa bado yuko hai na anaendelea vizuri.

Bloga mmoja kutoka Kenya aliibua hofu mitandaoni kwa kusambaza taarifa za upotoshaji kuhusu hali ya rais huyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ililaani uvumi huo na kuwaomba wananchi wasisambaze habari ambazo hazijathibitishwa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »