John Maina: Familia ya Kasisi wa Kanisa Katoliki Aliyeuawa Baada ya Kumkaribisha Gachagua Yazungumza

John Maina: Familia ya Kasisi wa Kanisa Katoliki Aliyeuawa Baada ya Kumkaribisha Gachagua Yazungumza

  • Sarah Wambui alisema kuwa Padre John Maina Ndegwa alikuwa mtu mwenye nidhamu na heshima tangu akiwa mtoto
  • Kwa machozi, mama huyo aliyevunjika moyo alisema ameacha kila kitu mikononi mwa Mungu, ambaye ana uwezo wa kuleta haki kwa familia hiyo
  • Babake Maina alisimulia kwa uchungu maneno ya mwisho ya mwanawe hospitalini huku akikumbuka hali aliyopatikana akiwa ameuawa

Familia iliyogubikwa na majonzi yake padri wa Kanisa Katoliki aliyefariki dunia kwa mazingira tatanishi ilizungumza wakati wa mazishi yake.

John Maina: Familia ya Kasisi wa Kanisa Katoliki Aliyeuawa Baada ya Kumkaribisha Gachagua Yazungumza
Sara Wambui (kushoto) anaomboleza mwanawe Padre John Maina Ndegwa (kulia). Picha: TV47 Kenya, Radio 47.
Chanzo: Youtube

John Maina Ndegwa anadaiwa kuuawa wiki chache baada ya kumkaribisha Naibu Rais wa zamani, Rigathi Gachagua.

Padre huyo alimkaribisha mwanasiasa huyo kama mgeni maalum katika sherehe ya Siku ya Familia ya Igwamiti Parish iliyofanyika kwa mara ya 25.

John Maina Ndegwa alizikwa lini?

Padre Maina alizikwa katika hafla ya maombolezo yaliyoshamiri majonzi mnamo Alhamisi, Mei 22, katika Kituo cha Kiroho cha Tabor Hill.

Sara Wambui alipata ugumu wa kukubaliana na kifo cha mwanawe, ambaye alikuwa sehemu muhimu ya familia.

“Machozi ninayomwaga ni kwa ajili ya watoto. Nimeacha kila kitu mikononi mwa Mungu kwa sababu najua Yeye anafanya kazi. Anaweza kufanya chochote, na anafanya. Mshukiwa ajitokeze, kwa sababu najua Mungu wangu ana uwezo, na itatendeka—yatakayompendeza kufanya. Si kwa mkono wa mwanadamu, bali kwa mkono Wake.

Sina mengi ya kusema kwa sababu najihisi vibaya na nimejeruhiwa. Niko katika maumivu na siwezi kujieleza jinsi ningependa. Hili si jambo rahisi,” alisema.

Babake John Maina Ndegwa afunguka kuhusu mwanawe wakati akiwa mchanga

Wambui alielezea tabia ya mwanawe alipokuwa mdogo, akisema kuwa Maina alikuwa mvulana mwenye nidhamu.

Subscribe to watch new videos

Hatujasikia malalamiko yoyote kwamba mwanawe aliwahi kumuumiza au kumkosea mtu yeyote, wala kuwa na matatizo na yeyote.

Babake Maina, akiwa katika majonzi, alisimulia wakati wake wa mwisho na mwanawe, ambaye chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika.

“Walimpa kitu kisichofaa. Maneno yake ya mwisho yalikuwa, ‘Wamenilisha kitu.’ Na huo ukawa mwisho. Baada ya kusema hivyo, hakuongea tena. Tulipoangalia kichwa chake, kilionekana kupigwa mara kadhaa. Nguo zake zilionekana kama zilichanwa. Hata kiatu chake kimoja kilikuwa kimechanika. Ilionekana kama alikuwa akibururwa na kitu,” alisimulia.

Kulingana na familia, Maina alionekana kwa mara ya mwisho akiendesha gari aina ya double-cabin kuelekea Mary Immaculate Cathedral Parish, ambalo ni kanisa kuu la Dayosisi ya Nyahururu, mnamo Jumatano, Mei 14, saa 4 asubuhi.

Siku iliyofuata, alipatikana akiwa hai lakini katika hali mahututi na dereva wa bodaboda barabara ya Kikopey kuelekea Nakuru, na alikimbizwa katika Hospitali ya St. Joseph.

Wafanyakazi wa Parokia ya St. Louis Igwamiti, waliokuwa wakihangaika kukubaliana na kifo cha padri wao, walisema kuwa Maina aliondoka kwa gari lake peke yake majira ya saa 5 asubuhi.

John Maina: Familia ya Kasisi wa Kanisa Katoliki Aliyeuawa Baada ya Kumkaribisha Gachagua Yazungumza
Mazishi ya Padre John Maina Ndegwa Nyahururu. Picha: Radio 47.
Chanzo: Facebook

John Maina Ndegwa azikwa Nyahururu

Katika simulizi nyingine, wingu la huzuni lilitanda katika Parokia ya Igwamiti, Nyahururu, huku padri aliyeuawa akiwekwa kwenye nyumba yake ya milele.

Mamia ya waombolezaji walihudhuria hafla hiyo ya kihisia kumzika mpendwa wao na mtumishi wa Mungu.

Jambo moja lililogundulika ni kutokuwepo kwa Rigathi Gachagua, ambaye alikuwa mgeni wa padri huyo wiki chache kabla ya kifo chake.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »