Mwanamke Asimulia Jinsi Alivyokamatwa Pamoja na Wanawe, Kudhulumiwa Msituni Sababu ya Mzozo wa Ardhi
- Hilda Muthoni Ndira na watoto wake wachanga walinyanyuliwa kwenda msitu katika kaunti ya Embu na watu waliowajua
- Walifungwa kwenye miti tofauti huku watoto wakishuhudia mama yao akidhulumiwa mbele yao
- Akizungumza na TUKO.co.ke, Muthoni, kutoka kaunti ya Kirinyaga, alidai alikuwa na mgogoro na mjomba wake, ambaye alimtuhumu kuwa aliwapa watu hao fedha kumdhalilisha
Mwanamke mchanga kutoka kaunti ya Kirinyaga ameonyesha hisia zake kuhusu mateso aliyoyapata mikononi mwa mjomba wake.

Chanzo: Original
Hilda Muthoni Ndira alidai kuwa amepitia kipindi kigumu sana kutokana na mgogoro wa ardhi na kaka wa marehemu mama yake.
Mama huyo wa watoto wawili alisema nusra apoteze maisha yake kutokana na mzozo wa ardhi.
Akizungumza na TUKO.co.ke, Muthoni alifichua kuwa alijulishwa kuhusu mpango wa mjomba wake kuuza kipande cha ardhi, jambo lilimfanya aanze kutafuta haki yake.
“Nilienda kijijini ili kumwomba mjomba wangu anipe kipande cha ardhi. Nilimwomba mkuu wa kijiji ambaye akamuita mjomba wangu. Chifu aliomba rushwa ili amsaidie katika suala hilo. Baadaye nilienda kwa Kamishna wa Wilaya (DC), ambaye alimwita mzee wa kijiji. Kulikuwa na mizunguko mingi. Mwanamke aliyefanya kazi ofisini kwa DC alinipa nambari ya Kamishna wa Kaunti na kuniambia nisiondoke ofisini kwake hadi nipate msaada,” alisema.
Muthoni alitembelea ofisi ya Kamishna wa Kaunti ambapo afisa huyo aliahidi kuangalia kesi yake na kuwasiliana na chifu wa kijiji pamoja na DC.
Muthoni apatiwa makazi na chifu
Kamishna wa Kaunti aliagiza mzee wa kijiji kumpatia Muthoni mahali pa kulala wakati kesi yake ikiendelea kutatuliwa siku zilizo fuata.
“Nilikuwa nikifua nguo zangu wakapita watu watatu, wakarudi, wakanisalimia na kusema wametumwa na chifu, wakadai kuna hati za ardhi nahitaji kusaini na wakasema kuna gari linanisubiri, nilipoingia ndani niliona visu na mapanga vimefichwa chini ya mkeka mweusi, wakavitoa na kuniambia nikae kimya nisiseme neno.
Tuliendesha gari hadi tukapita bango lililoandikwa ‘Karibu Embu.’ Kulikuwa na msitu karibu, na huko ndiko walikonipeleka mimi na watoto wangu. Walinitesa, wakiniuliza nilikuwa natafuta nini Kirinyaga na kwa nini nilitaka ardhi hiyo. Walinionya nisiulize tena kuhusu ardhi hiyo. Walinichoma kisu na kuniacha nikivuja damu, huku watoto wangu wakinitazama,” alikumbuka kwa uchungu.

Chanzo: Original
Watoto wa Muthoni washuhudia mama yao akiteseka wasijue la kufanya
Ilikuwa ni wakati wa kusikitisha sana kwani watoto wadogo wa Muthoni waliangalia kwa machozi wakati mama yao alikuwa akiteseka.
Kwa bahati nzuri, wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakipita walisikia kilio cha msaada.
"Walikuja wakanichukua na kunikimbiza hospitalini, nilikuwa nimepoteza damu nyingi kutokana na mateso hayo. Nilipelekwa katika Hospitali ya Embu Level 5, ambako nilikaa karibu miezi saba katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU). Sikujua waliko watoto wangu kama walikuwa wanakula au walikuwa wanawahudumia. Sikujua chochote," alisema huku akitokwa na machozi.
Mwanaume kutoka Machakos aharibu nyumba ya wazazi wake kutokana na mzozo wa ardhi
Katika hadithi nyingine, mwanamume wa umri wa kati alidaiwa kuharibu nyumba ya wazazi wake katika Kaunti ya Machakos, eneo la Masinga.
Wakazi waliambia TUKO.co.ke kwamba mwanaume huyo asiye na ajira alikasirika baada ya kuku wa wazazi wake kuingia ndani ya nyumba yake.
Mwanaume huyo ambaye hana mke pia alidaiwa kuwa na mzozo wa muda mrefu wa ardhi na wazazi wake.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke