Familia Yaingiwa na Hofu Mwanafunzi wa Darasa la 9 Kutoweka Alfajiri, Sare Yake Yapatikana

Familia Yaingiwa na Hofu Mwanafunzi wa Darasa la 9 Kutoweka Alfajiri, Sare Yake Yapatikana

  • Msichana wa miaka 14, Mary Maureen Wanjiru Kimani, alitoweka nyumbani kwao Rironi, Kaunti ya Kiambu, asubuhi ya Mei 21, 2025
  • Mary aliamka kama kawaida saa kumi na moja alfajiri kujiandaa kwenda shule, lakini alipotea kabla ya mamake kuamka nusu saa baadaye
  • Familia hapo awali ilidhani alikwenda shule, lakini shule ilithibitisha kuwa hakuwasili; amekuwa akitafutwa kwa wiki mbili sasa

Familia iliyohuzunika kutoka Kiambu sasa inaomba msaada kumpata binti yao wa miaka 14 aliyeoweka mapema asubuhi ya Mei 21, 2025.

Familia Yaingiwa na Hofu Mwanafunzi wa Darasa la 9 Kutoweka Alfajiri, Sare Yake Yapatikana Karibu
Msichana huyo wa Kiambu alitoweka wiki mbili zilizopita.
Chanzo: UGC

Msichana mdogo wa Kidato cha Tisa, aliyetambuliwa kama Mary Maureen Wanjiru Kimani, alitoweka majira ya saa kumi na alfajiri katika eneo la Rironi, Kaunti ya Kiambu, wiki mbili zilizopita, baada ya kuamka kama kawaida kujiandaa kwenda shule.

Akizungumza na TUKO.co.ke, babake alieleza kuwa msichana huyo aliamka mapema, akavaa sare ya shule kama ilivyo desturi yake asubuhi, lakini wakati mamake aliamka saa kumi na moja unusu alfajiri, Mary hajulikani popote.

"Alikuja kuniambia kuwa binti yetu hakuwepo na tayari alikuwa ameondoka. Nilijaribu kupiga simu shule kuuliza kama alikuwa amefika, lakini tuliambiwa hakuwa shuleni. Baada ya saa kadhaa za kumtafuta kila mahali, nilienda kwa chifu kupiga ripoti. Pia nilienda kituo cha polisi cha Limuru kuripoti kutoweka kwake," baba alisema.

Baadaye, alipigiwa simu na kuambiwa kuhusu kugunduliwa kwa sare ya shule ya binti yake, mita chache tu kutoka nyumbani kwake.

"Binti yangu alikuwa akisoma katika Shule ya Msingi ya Nyoro huko Rironi, na nilipigiwa simu na kuambiwa kuwa sare yake ya shule ilipatikana barabarani, mita chache tu kutoka nyumbani kwetu. Inaonekana alitoka nyumbani akiwa na sare na kubadilisha nguo nyingine baada ya kutoka," alieleza.

Wazazi pia waligundua kuwa baadhi ya nguo za msichana huyo zilikuwa hazipo.

"Tumemtafuta kila mahali kwa matumaini kuwa tutampata. Nimeongea na marafiki na familia wakisaidia kumtafuta. Imekuwa wiki mbili sasa na tuna wasiwasi mkubwa. Yeyote aliye na taarifa zozote kuhusu alipo anaweza kunipigia," alisema.

Ikiwa una taarifa yoyote kuhusu aliko Mary, tafadhali wasiliana na familia kupitia 0710775112 au 072369037 / 0785151784, au ripoti kwa kituo cha polisi kilicho karibu nawe.

Mama kutoka Kakamega aomba msaada baada ya mwanawe kutoweka

Katika habari nyingine, mama mmoja kutoka Kakamega aliomba msaada baada ya mwanawe, Clinton Mengo, kutoweka jana.

Mama huyo alisema kuwa mwanawe aliondoka nyumbani baada ya kumkaripia kwa kurudia makosa yale yale licha ya kuonywa awali.

Alieleza kuwa kijana huyo aliacha barua ya mkono mezani, akiomba msamaha na kueleza kuwa mamake asijaribu kumtafuta.

Katika barua hiyo, kijana huyo alisema kwa msisitizo kuwa angerudi nyumbani tu ikiwa na wakati ambapo tabia yake ingekubalika na mamake.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »