Kitendawili baada ya Mume na Mke Kupatikana Wamefariki Nyumbani Kwao Katika Mazingira ya Kutatanisha

Kitendawili baada ya Mume na Mke Kupatikana Wamefariki Nyumbani Kwao Katika Mazingira ya Kutatanisha

  • Geofrey Anael Mota na mkewe Blandina Felix Ngowi walipatikana wamefariki ndani ya nyumba yao katika kata ya Msaranga, manispaa ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania
  • Wawili hao hawakutoka nyumbani kwao siku nzima na walikutwa wamekufa kitandani mwao, hali iliyowaacha wakazi wakiwa na mshtuko na majonzi
  • Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, kupitia Kamishna Mwandamizi wa Polisi Simon Maigwa, lilieleza kuwa Anael alikuwa na majeraha ya wazi shingoni

Wakazi wa kata ya Msaranga, manispaa ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania wamejaa hofu na wasiwasi kufuatia kifo cha wanandoa wakongwe.

Kitendawili baada ya Mume na Mke Kupatikana Wamefariki Nyumbani Kwao Katika Mazingira ya Kutatanisha
Mwanaume Mtanzania Geofrey Anael Mota (kulia) na mkewe Blandina Felix Ngowi (kulia) waliokutwa wamekufa nyumbani kwao. Picha: Global TV Online.
Chanzo: Youtube

Geofrey Anael Mota na mkewe Blandina Felix Ngowi wanadaiwa kuuawa usiku ndani ya nyumba yao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, mwili wa marehemu Mota ulikutwa na jeraha kubwa shingoni.

Inaaminika kuwa jeraha hilo lilisababishwa na kukatwa kwa kitu chenye ncha kali, tofauti na mwili wa mkewe ambao haukuonyesha majeraha ya nje yanayoonekana.

Mtoto wa wanandoa hao wa Tanzania atoweka baada ya kifo chao

“Tukio lilitokea usiku wa Alhamisi kati ya saa 12 na saa saba usiku. Nilipofika, nilikuta polisi. Dada yangu alikuwa amelala kitandani, baba yangu alikuwa na majeraha kichwani na shingoni, na mamangu alikuwa amefunikwa na damu. Walikuwa wakiishi na mdogo wangu, ambaye hakuwepo kabisa baada ya tukio hilo. Hadi sasa bado hatujampata. Mahali alipo bado ni kitendawili,” alisema Abraham Jota, mwana wa marehemu.

Juhudi zinaendelea ili kumtafuta mdogo wa Jota—ambaye jina lake limebanwa kwa sababu za kisheria—ili kusaidia katika uchunguzi wa tukio hilo lililozua taharuki kwa jamii ya Msaranga.

Kamishna Maigwa aliwahakikishia wananchi kuwa uchunguzi wa awali unaofanywa na vyombo vya upelelezi unaendelea kwa kina ili kubaini chanzo cha tukio na wahusika.

Katika maendeleo yaliyotia mashaka, kijana huyo—mwana wa marehemu—anadaiwa kutoweka mara moja baada ya tukio hilo kutokea.

Subscribe to watch new videos

Eliud Athumani Mshana azungumza kuhusu mauaji ya wanandoa hao

Eliud Athumani Mshana, mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Msufini, kata ya Msaranga, alisema kuwa marehemu walikuwa nyumbani kwao siku nzima.

Alikiri kuwa muuaji wa tukio hilo la kutisha bado hajajulikana, lakini alidai kuwa huenda kijana wa wanandoa hao alihusika na tukio hilo.

“Kijana huyo, kwa bahati mbaya, alikuwa na matatizo ya akili. Hakuwa mtu wa ugomvi, lakini kutoweka kwake kunaashiria kuwa anahusika kwa namna fulani,” alisema.

Dadake Mota alisisitiza kuwa kakake hakuwa na matatizo na mtu yeyote—hata si mke wake—ambayo yangeweza kusababisha kifo cha kikatili kama hicho.

Wakenya waguswa na vifo vya wanandoa hao wa Tanzania

Watu katika mitandao ya kijamii waligubikwa na huzuni wakitoa maoni yao:

AnnamaDavid-e7n:

“Sie wengine ambao hatuna baba wala mama huwa tunawatamani sana nyie mliojaliwa kuwa na wazazi. Tunaomba muwatunze.”

Asha-s9u8p:

“Wengine tunawatafuta wazazi, wengine wanawaua. Ni bora kama walimuudhi angeenda kuishi mbali, siku akiwakumbuka anarudi, kuliko kuwaua.”

shamilafaraj5146:

“Huenda sio mtoto. Kuna mtu tu kapanga mipango yake kwa akili ili wamdhanie huyo mtoto. Mungu anajua nini kimewapata.”

JackriniMushi:

“Poleni sana.”

JenniferJacob-hh3ij:

“Huenda hata sio yeye, labda wauwaji wameondoka naye.”

msangi-d3f:

“Kaua wazazi jameni. Hapo itakuwa hana akili. Kwa nini akimbie basi?”

Kitendawili baada ya Mume na Mke Kupatikana Wamefariki Nyumbani Kwao Katika Mazingira ya Kutatanisha
Picha: Dadake Geoffrey Mota akizungumza baada ya kifo cha kaka yake. Chanzo: Global TV Online.
Chanzo: Youtube

Mume wa Hannah Wangare afikishwa mahakamani

Huku nyumbani Kenya, mume wa mfanyakazi wa M-Pesa aliyeuawa mjini Nakuru, alifikishwa mahakamani Jumanne, Juni 3, baada ya kuhusishwa na mauaji ya mkewe, Hannah Wangare.

Polisi wanaamini kuwa Zachariah Wambugu Wanjohi alihusika katika kutoweka na hatimaye kuuawa kwa mkewe.

Afisa mmoja aliieleza mahakama kuwa simu ya Wanjohi ilionekana maeneo yaleyale ambapo simu ya marehemu ilituma ishara yake ya mwisho.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

OSZAR »