Mzungu Mwanamke Aliyemtema Mumewe Baada ya Kupendana na Barobaro wa Kimaasai Mombasa Asema Anajuta

Mzungu Mwanamke Aliyemtema Mumewe Baada ya Kupendana na Barobaro wa Kimaasai Mombasa Asema Anajuta

  • Mwanamke Mzungu kwa jina Cheryl Thomasgood kutoka Isle of Wight, Uingereza, alimuacha mumewe na watoto kwa ajili ya barobaro wa miraba minne kutoka Kenya
  • Aliacha maisha ya kifahari Uingereza na kusafiri kuanza kuishi kwenye manyatta, akila damu, kabeji, na baadaye wakapata mtoto
  • Walipofika Uingereza, Lakimencho kwa bahati mbaya alibadilika na kuwa na tamaa ya pesa kupita kiasi, akawa na kasumba ya kutuma pesa nyumbani, hivyo wakatengana

Uingereza: Mwanamke Mzungu aliyemuacha mumewe ili kuwa na mpenzi mpya anasema anajutia sana uamuzi huo baada ya jamaa kubadilika, kupenda pesa kupita kiasi, na hatimaye ndoa yao kuvunjika.

Mzungu Mwanamke Aliyemtema Mumewe Baada ya Kupendana na Barobaro wa Kimaasai Mombasa Asema Anajuta
Mzungu Mwanamke Aliyemtema Mumewe Baada ya Kupendana na Barobaro wa Kimaasai Mombasa Asema Anajuta
Chanzo: UGC

Walikutana vipi?

Daily Mail iliripoti kuwa Cheryl Thomasgood, mwenye umri wa miaka 65 na aliyeishi Isle of Wight, aliacha mumewe na watoto wao watatu ili kuolewa na mwanamume wa Kisamburu mwenye haiba anayeitwa Daniel Lakimencho, aliyekuwa akiishi kwenye manyatta.

Wawili hao walikutana Cheryl alipokuja likizoni katika hoteli ya Bamburi Beach mjini Mombasa, ambako Lakimencho alikuwa sehemu ya kikundi cha kitamaduni kilichokuwa kikitumbuiza watalii.

"Nilidhani nimepata roho pacha wangu," Cheryl aliambia Daily Mail Online.

Wakati Cheryl alikuja Kenya kwa likizo, alikuwa na umri wa miaka 34, ameolewa na mume wake wa pili Mike Mason, na walikuwa wakilea watoto watatu.

Hata hivyo, ndani ya wiki chache baada ya kukutana na Lakimencho, maisha yake yalibadilika kabisa.

Mzungu Mwanamke Aliyemtema Mumewe Baada ya Kupendana na Barobaro wa Kimaasai Mombasa Asema Anajuta
Daniel Lakimnecho na Cheryl Thomasgood walipokuwa wapenzi. Picha: Daily Mail.
Chanzo: UGC

Aliamua kuvunja ndoa yake na kurudi Kenya kuwa na mpenzi wake mpya.

Alibadilisha maisha ya starehe kwa ugumu wa maisha ya manyatta—vitanda vya ngozi ya mbuzi, damu ya ng'ombe, na mboga za kabeji.

Baadaye walifunga ndoa na kurudi Uingereza ili binti yao, Mitsi, aweze kukua karibu na watoto wengine wa Cheryl.

Hata hivyo, mambo yalibadilika walipofika Uingereza. Lakimencho, ambaye awali alikuwa mtu wa kiroho na rahisi, alianza kuwa na tamaa ya pesa, mali, na kutuma fedha nyumbani.

Cheryl Thomasgood yuko wapi sasa?

Mwaka moja baada ya kuzaliwa kwa Mitsi, walianza kugombana na hatimaye wakatengana.

Kwa sasa, Cheryl anaishi peke yake katika mji wa pwani wa Somerset, ambapo majirani wake wengi hawajui kuhusu maisha yake ya zamani.

Kwa sasa anajuta sana kwa athari ambazo vitendo vyake vilisababisha kwa watoto wake. Hana mawasiliano yoyote na Lakimencho, lakini ana uhusiano wa karibu sana na watoto wake.

Anamchukulia Mitsi kama “kitu kizuri pekee” kilichotokana na ndoa hiyo iliyoshindikana.

"Nilikuwa kwenye kipindi kigumu, nikafikiri Daniel angeniponya. Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa nikikimbia matatizo yangu. Haikuwa mapenzi—ilikuwa ni njia ya kutoroka," alisema.

Kile kilichoanza kama mapenzi yaliyoivuka mipaka ya tamaduni na mabara sasa ni hadithi ya majuto, kuvunjika moyo, na funzo maishani.

Jamaa Anayechumbiana na Mzungu Mkubwa Amfunguka

Katika hadithi nyingine, Dangote Kenya, ambaye kwa sasa anaishi Diani, alieleza jinsi alivyokutana na mwanamke mzungu mkubwa kwake kiumri.

Wakati mmoja, waligombana kuhusu kipindi walichokuwa kwenye uhusiano, jambo lililomfanya mwanamke huyo aonyeshe hasira kidogo.

Alimkemea na kumkumbusha kuwa wamekuwa pamoja kwa miezi mitatu, kisha akauliza kama angetaka amrudishe shule.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

Vichwa:
OSZAR »