Mama wa Nakuru Asimulia kwa Machozi Kifo cha Kutatanisha cha Bintiye Baada ya Kuachana na Kanisa
- Monica Mwangi kutoka Molo, kaunti ya Nakuru, alipoteza binti yake Njoki katika mazingira ya kutatanisha
- Mama huyo mwenye huzuni aliambia TUKO.co.ke kwamba alihisi huzuni isiyoelezeka na kulia mara kwa mara wiki mbili kabla ya kifo cha ghafla cha binti yake
- Alidai kwamba kanisa pamoja na nabii wake huenda walihusika katika kifo cha binti yake, akitaja sababu kadhaa
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Mwanamke mmoja kutoka Molo, kaunti ya Nakuru, amesimulia kwa uchungu jinsi binti yake alivyofariki katika mazingira ya kutatanisha.

Chanzo: UGC
Katika mahojiano ya kipekee na TUKO.co.ke, Monica Mwangi alisimulia kuwa alikuwa ameacha kuhudhuria kanisa moja jijini Nairobi linaloendeshwa na nabii wa kike, muda mfupi kabla ya kumpoteza binti yake, Njoki.
Alieleza kuwa kujiunga na kanisa hilo kuliharibu maisha yake binafsi, biashara yake, na hata kuliathiri masomo ya binti yake.
“Ilikuwa Desemba 23, 2023, na binti yangu ambaye alikuwa na biashara ya matunda na upishi baada ya kuacha shule alikuwa kazini, lakini tulikuwa tumekubaliana kuwa atarudi nyumbani saa 11 jioni kwa ajili ya chakula cha usiku,” alisema Monica.
Monica alisema kuwa binti yake alikuwa na furaha wakati huo, huku sikukuu ya Krismasi ikikaribia, lakini yeye binafsi alihisi huzuni isiyoelezeka.
“Wiki mbili kabla ya siku hiyo, kitu fulani kilikuwa kinanifanya nilie sana. Sikuwa najua ni nini, lakini nilikuwa nalia tu bila sababu,” aliongeza.
Licha ya hisia hizo mbaya, alikuwa akitarajia kutumia jioni hiyo vizuri na Njoki, ambaye alifika nyumbani akiwa na furaha, mwenye bashasha.
Monica alieleza kuwa aliandaa chakula cha jioni kwao wawili, huku binti yake akishiriki habari njema kuhusu wateja waliokuwa wamemkabidhi kazi ya upishi kwa ajili ya Krismasi.
Waliendelea kuzungumza na kufurahia supu ya kuku Monica aliyopika, kisha Njoki akaenda kuoga.
Alikumbuka kuwa binti yake alionekana mwenye afya njema, mwenye furaha, na akitarajia kwa hamu kusherehekea sikukuu hiyo.
“Nilienda kulala. Kisha, dakika kama kumi kabla ya saa saba usiku, nilisikia sauti kama ya bomu ndani ya nyumba. Niliruka kitandani na kukimbilia mahali sauti ilipotokea, na hapo nikamkuta Njoki akiwa ameanguka sakafuni,” alisema Monica kwa uchungu.
Alipiga kelele na kuita msaada, majirani walifika na kumkimbiza Njoki hospitalini.
“Nilimwita kwa jina lake lakini hakuitika. Madaktari walisema walijaribu kadri ya uwezo wao, lakini alifariki tu ghafla,” alisema Monica kwa huzuni.

Chanzo: UGC
Nini kilimfanyikia bintiye Monica Mwangi?
Mwaka moja na miezi sita baadaye, Monica bado anajiuliza kilichomsibu binti yake mpendwa.
Alidai kifo cha Njoki kinahusiana na nabii huyo wa kike, ambaye alimfilisi kihisia na kifedha.
“Tangu nilipoondoka kanisani, hakuna aliyenitembelea. Kisha siku mbili baada ya kifo cha binti yangu, wote walijitokeza wakitaka kuongoza ibada ya mazishi na kununua jeneza,” alisema Monica.
Monica alisema kuwa nabii huyo alidai kuwa Njoki alimtokea kwenye ndoto wiki moja kabla ya kifo chake, jambo lililomfanya mama huyo ajiulize iwapo kifo cha binti yake kilikuwa cha kawaida au kilisababishwa na uchawi.
Alisema kuwa huenda yeye ndiye alikuwa amelengwa kutokana na siri alizonazo, lakini kifo kikampata binti yake badala yake.
“Kuna mwanamke mwingine aliyekufa baada ya kuacha kanisa hilo, kama mimi. Alijiunga na kanisa jingine, akafa, kisha nabii huyo akakimbilia tena kununua jeneza. Swali langu ni: kwa nini anafanya hivyo? Hiyo ni ushahidi wa kutosha kwangu kwamba anahusika. Amewafunga watu wa kanisa hilo; wanazidi kumpa pesa,” aliongeza.
Mke wa mchungaji wa Nairobi adaiwa kuiba KSh 284,000
Katika taarifa nyingine, TUKO.co.ke iliripoti kuwa mke wa mhubiri mmoja jijini Nairobi amejipata matatani baada ya kudaiwa kufuja fedha za mazishi.
Arich Ndege alidai kuwa mke huyo wa mchungaji aliiba KSh 284,000, ambazo alielekeza kwa matumizi yake binafsi badala ya kuenzi kumbukumbu ya marehemu.
Familia ya marehemu ilitishia kwenda hadharani na kuwasilisha ushahidi wa udanganyifu huo iwapo haki haitatendeka.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke