Albert Ojwang: Picha 5 za Mjane Mchanga wa Bloga Aliyeuawa
- Marehemu bloga Albert Ojwang ameacha mjane mchanga sana aitwaye Nevnine Onyango pamoja na mtoto
- Albert alimtambulisha kwa wazazi wake mwezi Aprili, miezi miwili kabla ya kifo chake cha kusikitisha akiwa mikononi mwa polisi
- TUKO.co.ke imechunguza maisha ya Nevnine na makala haya yanaangazia mambo ya kufurahisha kuhusu dada huyu mtulivu
Kifo cha bloga Albert Ojwang akiwa mikononi mwa polisi kimeitikisa nchi, huku Wakenya wazalendo wakimiminika mitaani kuandamana wakitaka haki itendeke.

Chanzo: Twitter
Wengi pia wamejitokeza kuiunga mkono familia hiyo, wakitoa msaada wa kifedha na kihisia.
Mjane wake mchanga, Nevnine Onyango, pia amepokea msaada huo na kuwa mtu wa kuvutia umma.
TUKO.co.ke imemshirikisha kupitia picha zake na baadhi ya mambo ya kuvutia ambayo hukuyajua kuhusu sura yake tulivu na ya kupendeza.

Chanzo: Facebook
1. Ni kwa muda gani Albert Ojwang na Nevnine Onyango waliishi pamoja?
Wawili hao hawakuishi pamoja kwa muda mrefu kama wanandoa, kwani Ojwang alimtambulisha Nevnine kwa wazazi wake mwezi Aprili, miezi miwili kabla ya kifo chake.
Walikuwa wamechumbiana kabla ya hapo na wakakubaliana kufunga ndoa rasmi.
Wakati Ojwang alimtambulisha mkewe kwa familia yake katika kijiji cha Kakoth, eneo bunge la Kabondo Kasipul, walipokelewa kwa furaha.
Wanandoa hao waliishi katika nyumba ndogo ya Ojwang (simba) kulingana na mila za Wajaluo.

Chanzo: Instagram
2. Nevnine Onyango ana tabia gani?
Mjane huyo kijana amekuwa akionekana kwenye vyombo vya habari tangu kifo cha Albert, na kwa sasa kila mtu ana mtazamo wake kuhusu mwenendo wake.
Nevnine ni mtu mtulivu na mwenye nidhamu. Amedhibiti hisia zake kikamilifu licha ya majonzi makali ya msiba alioupata.
3. Nevnine Onyango anashabikia timu gani ya kandanda?
Wengi wa wanawake hawapendi kandanda, lakini hali ni tofauti kwa Nevnine.
Anapenda Ligi Kuu ya Uingereza na ni shabiki sugu wa Manchester City.
Nevnine haoni aibu kuonyesha kuwa ni shabiki wa Manchester City, jambo linaloonekana wazi kwenye akaunti yake ya Facebook.
Kwa upande mwingine, marehemu mumewe, Albert, alikuwa shabiki mkubwa wa Manchester United.

Chanzo: Facebook
4. Nevnine Onyango anaamini nini kidini?
Nevnine, ambaye sasa amebaki na mtoto mmoja, ni Mkristo.
Katika akaunti yake ya Facebook, amejiita "binti kipenzi wa Mungu."

Chanzo: Twitter
5. Nevnine Onyango alizaliwa lini?
Mrembo huyo huwa anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa kila mwaka kupitia Facebook.
Siku ya kuzaliwa ya Nevnine ni Agosti 25. Ingawa mwaka wa kuzaliwa haujawekwa wazi, inaaminika kuwa ana chini ya miaka 29. Makadirio yanaonesha kuwa anaweza kuwa na miaka 27.

Chanzo: Facebook
Ni swali gani ambalo mwana wa Albert Ojwang aliuliza?
Hapo awali, Nevnine alifichua kuwa mwanao mdogo, George Myles, alimuuliza kuhusu baba yake, Albert.
Kwa mujibu wa Nevnine, Myles alisema kuwa alikuwa amesikia watu wakisema kuwa baba yake amekufa, na akauliza mamake kama ni kweli.
Mjane huyo aliyekuwa akihuzunika hakujua jinsi ya kumjibu mwanawe mdogo.
Jumapili, Juni 15, Nevnine alishiriki mazungumzo ya faragha aliyokuwa nayo na Albert mtandaoni na kumuenzi.
Alifichua kuwa Albert alikuwa na mipango mizuri kwa ajili ya mwanao kwa Siku ya Baba, lakini kwa bahati mbaya, hakuwahi kuitekeleza.
Wakenya wengi walimfariji na kuungana naye kudai haki.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke