Jamaa Wanne wa Familia Moja Wafariki Kwenye Ajali Walipokuwa Wakielekea Harusini
- Familia moja katika kijiji cha Ngusero inaomboleza kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyogharimu maisha ya jamaa wao wanne waliokuwa wakisafiri kwenda harusini
- Ajali hiyo iliwasbabishia watu 29 majera na wengine 38 wakifariki dunia, wakiwemo wanandugu hao na wapangaji wao wanne
- Katika video moja, Abdallah Kiluvia, mshiriki wa familia hiyo iliyoandamwa na msiba, alisema kwa masikitiko ajali hiyo ni pigo kubwa mno kwwa familia
PAY ATTENTION: Flexible Payment Plans Available! Invest in Yourself & See the Return with Our Affordable Copywriting Course!
Wingu la huzuni limeigubika familia moja katika kijiji cha Ngusero, Kilimanjaro, Tanzania, kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyosababisha vifo vya jamaa wao wanne.

Chanzo: Youtube
Familia hiyo, pamoja na wapangaji wao sita, walikuwa wakisafiri kuelekea mjini Moshi kuhudhuria harusi ya jamaa yao wakati ajali hiyo ilipotokea.
Nini kilisababisha ajali ya Kilimanjaro?
Kwa mujibu wa Mwananchi Digital, ajali hiyo ilihusisha basi dogo lililokuwa limebeba wageni wa harusi na basi la kampuni ya Chanel One lililokuwa likielekea Moshi kutoka Tanga.
Magari hayo mawili yaligongana uso kwa uso na kulipuka moto huku abiria wakiwa bado ndani.
Kwa masikitiko makubwa, jumla ya watu 38 walipoteza maisha, huku wengine 29 wakijeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea eneo la Sabasaba mjini Same.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, alithibitisha tukio hilo, akibainisha kuwa watu 24 walikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Same, huku wengine watano wakielekezwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi.
Familia yaongea baada ya kupoteza watu 6
Abdallah Kiluvia, mmoja wa familia iliyopoteza jamaa wanne na wapangaji sita katika ajali hiyo, alisema kuwa asilimia 98 ya miili hiyo iliteketea kwa moto kiasi cha kutotambulika.

Chanzo: Facebook
Kiluvia alieleza kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa familia nzima kwani hawakupoteza tu ndugu zao bali pia wapangaji sita waliokuwa wameambatana nao kwa ajili ya harusi.
“Nimepoteza kakangu, mke wake, watoto wao wawili, na jamaa wengine wawili wa familia. Wote walikuwa wakielekea kwenye harusi ya mpwa wangu wakati ajali ilipotokea umbali wa kilomita 3 tu kutoka mji wa Same. Waliungua kiasi cha kutotambulika,” alisema Kiluvia.
Alisema kuwa wamekubali kuwa ni mapenzi ya Mungu na sasa wanasubiri matokeo ya vipimo vya DNA ili kusaidia kutambua miili hiyo na kuwapa mazishi ya heshima kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu.
Ramadhani Kiluvia, ambaye alipoteza mamake na mdogo wake, alisema alikuwa mjini Moshi akiandaa harusi hiyo ya jioni na alikuwa akiwangoja mamake na jamaa wengine wafike.
“Walianza safari yao majira ya saa kumi jioni na tulikuwa tukiwangoja kwa hamu. Nilipopokea simu nikaambiwa kuwa gari lililobeba familia yangu limehusika katika ajali. Nilikatiza simu mara moja na kujaribu kumpigia mama, lakini hakuweza kupokea,” alisema Ramadhani.
Mtoto huyo wa kwanza wa familia hiyo alikumbuka mazungumzo yake ya mwisho na mama yake kabla ya safari.
“Mimi ni mtoto wa kwanza na nilikuwa tayari katika ukumbi wa harusi. Mama aliniambia angekuja na wadogo zangu wawili, lakini sasa wote wamefariki,” aliongeza kwa uchungu mkubwa.
Familia kutoka Naivasha yaomboleza vifo vya watu 7 waliokufa kwenye ajali ya barabarani
Katika habari nyingine, TUKO.co.ke iliripoti kuwa watu saba wa familia moja waliaga dunia kwenye ajali mbaya ya barabarani katika barabara ya Naivasha–Longonot, kaunti ya Nakuru mnamo Machi 2025.
Miongoni mwa waliokufa walikuwa watoto watatu wa familia moja, mtoto mmoja wa mfanyakazi wa nyumbani, na watu wazima watatu waliokuwa ndugu.
Familia hiyo ilikuwa ikirejea nyumbani kutoka kwenye mazishi wakati gari lao lilipogongana uso kwa uso na gari lingine.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke