Nyeri: Afueni Baada ya Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Aliyetoweka kwa Wiki Moja Kupatikana Akiwa Hai

Nyeri: Afueni Baada ya Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Aliyetoweka kwa Wiki Moja Kupatikana Akiwa Hai

  • Kelvin Kamau Wandina, mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Upili ya Kianyaga Boys, alitoweka mnamo Juni 22 baada ya kuhudhuria ibada ya kanisani
  • Kutoweka kwake kuliwaacha familia yake katika hali ya wasiwasi mkubwa, na waliripoti tukio hilo mara moja huku wakianzisha msako wa kijamii
  • Kwa bahati nzuri, Kelvin alipatikana wiki moja baadaye saa tisa usiku akiwa mbali na nyumbani, huku familia yake ikieleza shukrani kwa wote waliowasaidia katika juhudi za kumtafuta

Familia moja ya Micha, kaunti ya Nyeri, sasa imepata afueni baada ya mwana wao aliyekuwa ametoweka kwa wiki moja kupatikana.

Nyeri: Afueni Baada ya Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Aliyetoweka kwa Wiki Moja Kupatikana Akiwa Hai
Familia ya Nyeri yapata afueni baada ya kumpata mwanao aliyetoweka. Picha: Karangu Muraya.
Chanzo: Facebook

Kelvin Kamau Wandina aliripotiwa kupotea mnamo Juni 22, muda mfupi baada ya kuhudhuria ibada ya kanisani katika eneo lao la nyumbani.

Familia yake iliwasilisha ripoti ya mtu aliyepotea katika kituo cha polisi cha eneo hilo na mara moja wakaanzisha juhudi za kumtafuta.

Walibaki wakiwa wamevunjika moyo na kujaa uchungu, wakijiuliza nini kingeweza kuwa kimemtokea, kwani alikuwa amerejea nyumbani kwa likizo ya kipindi cha katikati ya muhula (half-term).

Kelvin Kamau alipatikana wapi?

Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Upili ya Kianyaga Boys alipatikana siku ya Jumamosi, Juni 28, saa tisa alfajiri jijini Nairobi.

Kelvin alipatikana akiwa salama salimini na kwa sasa yuko mikononi mwa familia yake, akipata mapenzi na uangalizi wa jamaa zake.

Katika tangazo lililotolewa na familia yake wakiomba msaada wa kumtafuta, walimuelezea Kelvin kama mwanga uliokuwa uking’aa nyumbani kwao.

Walieleza hofu yao kutokana na ongezeko la visa vya vijana kupotea ghafla, na wakaomba msaada kutoka kwa Wakenya mitandaoni kuweza kumfuatilia kijana huyo.

“Kwa yeyote aliyenaye Kelvin Kamau Wandina, tafadhali, nakuomba kutoka kwenye kina cha moyo wangu, mrudishe nyumbani akaungane tena na wapendwa wake. Yeye ni mwana na kaka, na kutoweka kwake kumevunja familia yetu,” linasomeka tangazo hilo.

Nyeri: Afueni Baada ya Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Aliyetoweka kwa Wiki Moja Kupatikana Akiwa Hai
Kelvin Kamau alitoweka mnamo Juni 22.Picha: Karangu Muraya.
Chanzo: Facebook

Wanamitandao wafurahia kurejea kwa kijana wa Nyeri

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii walieleza furaha na shukrani zao kwa Mungu kwa usalama wake, huku wengine wakiwa na hamu ya kujua alikuwa wapi.

Joyce Mwangi:

“Halleluya, utukufu kwa Mungu! Hii ni ya ajabu machoni petu. Tunalitukuza jina la Bwana.”

Wairimu Liz:

“Alikuwa anafanya nini mahali alipokuwa?”

Esther Nyambura:

“Furaha na afueni kwa wazazi! Weuh, inaweza kuumiza sana moyo. Mungu ashukuriwe.”

Lucy Sandra:

“Wow, Mungu tunayemtumikia ni wa rehema kweli. Utukufu kwa Mungu Aliye Juu Sana. Bwana tunakushukuru kwa habari njema.”

Bianca Maish:

“Asante Mungu kwa kumrejesha huyu kijana jamani. Tuliomba arejee salama,

Mwanafunzi wa Nyamira aliyepotea apatika Eldoret

Katika habari nyingine, TUKO.co.ke iliripoti kuwa familia moja huko Nyamira ilifurahia baada ya binti yao, Mary Nyambeki, kupatikana.

Nyambeki alipotea baada ya kuondoka Shule ya Upili ya Wasichana ya Nyanchwa akielekea nyumbani kwa likizo ya katikati ya muhula.

Msichana huyo hakuwahi kufika nyumbani, jambo lililowatia hofu jamaa zake. Baadaye alipatikana mjini Eldoret.

Kutoweka kwa Nyambeki kulimchosha mama yake mpendwa ambaye alilazwa hospitalini kutokana na matatizo ya msongo wa mawazo (depression).

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Authors:
Shillah Mwadosho avatar

Shillah Mwadosho (Swahili editor) Shillah Mwadosho ni mwandishi wa habari wa TUKO.co.ke katika kitengo cha Kiswahili tangu 2019. Ana tajriba ya takriban miaka minne katika fani ya uandishi wa habari kwenye redio, televisheni na gazetini. Alipata ujuzi wa uanahabari katika taasisi ya Alphax mjini Eldoret. Yeye hujituliza kwa kusikiza muziki na kufurahia densi baada ya kazi. Email: [email protected]

Vichwa:
OSZAR »